Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega leo Aprili 27, 2024 ametembelea maeneo yalioathiriwa na mafuriko ya maji ya mvua katika jimbo la Mkuranga, mkoani Pwani na kufanya tathimini ni kiasi gani maeneo hayo yameathirika na kuona hatua za kuchukua ili kutatua changamoto hizo.


Katika ziara yake hiyo Mhe. Ulega ameanza kukagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko hayo ikiwemo barabara na madaraja katika kata ya Mwandege, Tambani, Vikindu, Mkuranga, Kiparang’anda, Mkamba, Kimanzichana, Nyamato na Lukanga.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi wanaokaa katika maeneo hayo yalioathiriwa na mafuriko kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kushughulikia changamoto hizo.







Share To:

Post A Comment: