Na. John Bera - ARUSHA
Leo tarehe 30 Aprili, 2024, Timu ya michezo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mwenyekiti wa Timu hiyo, Bi. Getrude Kassara pamoja na viongozi mbalimbali wa Timu hiyo wamekabidhi misaada ya hisani kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mei Mosi, Bi. Itika Mwankenja kwa ajili ya kuipeleka kwa wahitaji waliopo Mkoani Arusha ili iweze kuwasaidia.
Timu hii imedhihirisha ukarimu mkubwa kwa jamii kwa kuwasaidia watu wanaohitaji. Hatua hii ni mfano mzuri wa umoja na mshikamano katika kusaidia jamii kwa ujumla
Aidha, Wizara ya Maliasili na Utalii inajivunia kuwa na timu yenye moyo wa kujitolea ambapo mbali na kuhamasisha utalii wa michezo pia, inarudisha kwa jamii kwa namna moja au nyingine
Post A Comment: