Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania - TFS umetoa msaada wa kiasi cha shilingi 20,000,000/= kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko Wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani.
Akipokea msaada huo mapema hivi leo Mei 25, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge ameshukuru TFS kwa kujali wananchi wakati huu wa changamoto ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea.
"Fedha hizi zitatumika katika kutoa huduma kwa wananchi wanaopitia changamoto ya mafuriko Rufiji na Kibiti na ninaamini hiki mlichofanya kitaenda kutusaidia mbele kuhakikisha mazingira yanatunzwa,” alisema Mhe. Kunenga
Meneja Uhusiano wa TFS Johary Kachwamba akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa uhifadhi Prof. Dos Santos Silayo, amesema TFS inatoa pole kwa waathirika wa mafuriko kwa maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Rufiji na Kibiti,
"TFS ina misitu yenye hekta 32,902 ndani ya wilaya ya Rufiji, hivyo wana Rufiji ni Wahifadhi wenzetu na tutaendelea kuwashika mkono kipindi hiki cha changamoto ya mafuriko" Johary.
Post A Comment: