Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo tarehe 04 Aprili 2024 amepata nafasi ya katika kipindi cha kumekucha na ITV ambapo walijadili Mubashara Mikakati ya Kupambana na Udumavu katika mkoa wa Njombe.
Mhe. Mtaka alisema kuwa Mkoa umeanzisha Kampeni ya Lishe inayojulikana kwa jina la kampeni isemayo "Kujaza Tumbo si Lishe Jali Unachomlisha" yenye lengo la Kuwaelimisha Wazazi na walezi lakini pia na watoto ambao ndio taifa la kesho.
Aidha, alisema kuwa, hivi karibu mkoa unatarajia kuanza kufanya utafiti wa kina wenye lengo la kutambua hali ya udumavu kwenye Wilaya zote za Mkoa wa njombe na kupata taarifa zenye usahihi na uhalisia.
Wakazi wa Mkoa wa Njombe tayari wameanza kuelewa umuhimu wa uzingatiaji mlo kwa watoto chini ya miaka 5 na hata wamama wajawazito wanapata elimu wakiwa wajawazito na hata mara baada ya kujifungua ili wazingatie Lishe bora kwa wao wenyewe na kwa watoto wao.
Sambamba na hayo Mhe. Mtaka alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kushiriki Kipindi cha Malumbano ya hoja siku ya Kesho tarehe 04/04/2024 yatakayofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Post A Comment: