Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amekabidhi magari matatu kwa ajili ya wakuu wa wilaya za Rombo, Mwanga na Same, yenye thamani ya zaidi ya milioni 600 ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuleta maendeleo ya mkoa huo.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo nje ya viwanja wa ofisi za mkuu wa mkoa, Babu amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameanza kutekeleza maombi mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro ya kuwapatia Wakuu wa wilaya vitendea kazi.
Rc Babu amesema kuwa, Wabunge wamekuwa wakilalamika Bungeni kuhusiana na wakuu wa wilaya kukosa magari ambapo mkoa ulipanga kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu wawe wameshanunua magari matatu ya wakuu wa wilaya.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa, magari hayo yatatumika kwa ajili ya shughuli za kiserikali na kuwataka kwenda kuyatunza magari hayo kwani yamenunuliwa kwa gharama.
Post A Comment: