Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo ambaye pia alihudhuria Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo ya Misa Takatifu imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Matukio mbalimbali katika Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mama Fatma Karume Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume ambaye pia alihudhuria Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo ya Misa Takatifu imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024. Hayati Sokoine alifariki tarehe 12 Aprili, 1984 kutokana na ajali ya gari iliyotokea Wami Dakawa Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Post A Comment: