Na Denis Chambi, Tanga.
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2024 Godfrey Eliakimu Mnzava ameipongeza Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira 'Tanga Uwasa' kwa kuendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali katika kutangaza zabuni kupitia mfumo wa kisasa wa NEST unaozitaka mamalaka na taasisi zote hapa nchini kufanya hivyo ikiwa ni maelekezo yaliyotolewa ikiwa pia ni njia ya kudhibiti matumizi ya fedha za Umma.
Mnzava ametoa pongezi hizo wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru uliotembelea kukagua na kuzindua miradi miwili ya maji iliyopo wilaya za Tanga na Muheza inayosimamiwa na Tanga Uwasa' ambayo ilifadhiliwa na taasisi inayohusika na ulazaji wa bomba la mafuta ghafi linalotoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania ambapo amesisitiza na kuzitaka taasisi zote hapa nchini kutekeleza sheria ya manunuzi ya umma ambao unasaidia kuwapata wazabuni walio bora watakaowezesha kutekeleza miradi mbalimbali hapa nchini.
"Tumekagua nyaraka mbalimbali ambazo zinaonyesha utekelezaji wa miradi hii tumefurahishwa na jambo moja ambalo wenzetu hawa wameendelea kutekeleza maelekezo ya serikali ya kutangaza miradi na zabuni zote kupitia kwenye mfumo wa kisasa wa NEST tumeiona hii kazi nzuri iliyofanyika na Mwenge wa Uhuru umekagua na kuridhishwa na kilichofanyika"
"Tunaendelea kusisitiza kote nchini kwamba miradi yote ya maendeleo iwe ni ya fedha za kutoka Serikali kuu, wahisani, wadau wa maendeleo, michango ya wananchi hata kama ikiwa ni mapato ya ndani ya taasisi husika sheria ya kudhibiti matumizi ya fedha inatuelekeza zabuni zote zifanyike kupitia mfumo ili kudhibiti namna ya utoaji wa tenda na kuondoa ubaguzi kwa wakandarasi lakini pia ndio maelekezo ya sheria yamanunuzi ya umma" alisisitiza Mnzava.
Akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024 , msanifu wa miradi wa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira 'Tanga Uwasa" Mhandisi Violeth Kazumba kwenye mradi wa Chongoleani alisema kuwa katika no mradi ambao utawanufaisha wananchi wa kata tatu za Chongoleani, Mzizima na Mabokweni zenye wakazi 26,071 pia utawagusa wawekezaji , wafanyabiashara sambamba wafanyakazi wa taasisi inahohusika na ulazaji wa Bomba la mafuta ghafi linalotoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania.
"Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira inatekeleza mradi wa kuboresha miundombinu ya maji Safi katika maeneo ya kata tatu zenye mitaa 10 na wakazi 202,071 miundombinu inayojengwa katika mradi huu inakusudia kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo hayo lakini pia na watumiaji wengine kama viwanda na wafanyabiashara"
"Utekelezaji wa mradi huu ulianza November 2022 na kukamilika Machi 30, 2024 kwa asilimia mia moja mradi umefadhiliwa na taasisi inahohusika na ulazaji wa bomba la mafuta ghafi ambapo usanifu wake umekadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi Bilion 2,352,201,500 na hadi sasa mkandarasi ameshalipwa shilingi Bilion 1 ,823,766,540 sawa na asilimia 79.46"
Aidha katika mradi wa ambao unatarajiwa kunufaisha wakazi wapatao 21,721 kata za Genge, Lusanga Majengo na Tanganyika wilayani Muheza zenye zaidi wa pamoja na wafanyakazi wa eneo la mradi wa Bomba la mafuta ghafi 'EACOP' ukighalimu kiasi cha shilingi Million 532,550,000 ambapo kukamilika kwa mradi huo kumeendelea kurahisisha upatikanaji wa maji Safi na salama na kuwawezeaha kuondokana na adha ambazo wamekuwa wakikumbana nazo.
Akizungumza Mbunge wa Jimbo la Muheza mkoani Tanga ambaye pia ni naibu waziri wa utamaduni Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema kumekuwa na adha ya muda mrefu ya ukosefu wa maji ya uhakika kwaajili ya matumizi ya wananchi ambapo wamekuwa wakipata huduma hiyo mara moja kwa wiki hadi miezi miwili na sasa kukamilika kwa mradi huo kumetatua kwa asilimia kubwa changamoto hiyo.
"Ukosefu wa maji ni miongoni mwa kero kubwa ambazo zinaikabili wilaya ya Muheza tangu mwaka 2020 wananchi wa kata hizi walikuwa wanapata maji mara moja wakati mwingine inakwenda mpaka miezi miwili lakini sasa hivi tumefika mara tatu kwa wiki na hali inazidi kuimarika"
"Tuna mradi wa miji 28 na kwa wilaya ya Muheza katika mradi ule unakuja kunufaisha kata 17 tutapata Bilion 40 Kama fedha hizi hazitamaliza kero ya maji iliyopo kwa Sasa basi tatizo hili haliyoweza kuisha kabisa kazi kubwa inauofanywa na Serikali katika wilaya yetu inaonekana " alisema Mbunge huyo
Post A Comment: