Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Maliasili na Utalii inatarajiwa kesho tarehe 22.04. 2024 kutangaza rasmi matokeo ya sensa ya wanyamapori, Pamoja na kuzindua ripoti ya Watalii wa Kimataifa walioitembelea nchini kwa mwaka 2023.
Utangazaji na uzinduzi huu huo utajumuisha wadau mbalimbali wa uhifadhi na utalii utafanyika katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha, ambapo Waziri wa maliasili na utalii Angellah Kairuki ndiye anayetarajiwa kutangaza matokeo hayo ya sensa na kuzindua ripoti hiyo.
Katika mkutano wake na wanahabari jijini Arusha, Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Edward Kohi ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo amesema taarifa hizo zenye tija katika uhifadhi wa wanyamapori na kukuza utalii nchini zinaakisi juhudi za Serekali kuhifadhi utajiri wa Maliasili ya Wanyamapori na kukuza utalii nchini.
Aidha ripoti hiyo itaangazia matokeo watalii walioitembelea nchi hii mwaka 2023 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia filamu ya Royal Tour.
Post A Comment: