.
Kuelekea mashindano ya mpira wa miguu ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika ( AFCON ) yanayo tarajia kufanyika mwaka 2027 ambapo michuano hiyo inafanyika Jijini Arusha, Tayari maandalizi kabambe ya kuufanya mji huo kuwa Smart City katika nchi za Afrika kwa kuwalinda wageni wote na wananchi kiusalama.
Maandalizi hayo yakiwemo kufunga Camera a Kisasa za ulinzi katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha na kuendelea kutoa msaada mkubwa wa kiusalama kwa wananchi , pia maandalizi ya kujenga kiwanja cha mpira unaendelea pamoja na kurekebisha viwanja mbali mbali kwaajili ya mazoezi.
Akiongea na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Eng, Juma Hamsini, Ameeleza kuwa hadi sasa Kamera hizo walizo zifunga zimegharimu zaidi ya shilingi milioni mia mbili za kitanzania ( 200,000,000/=.) na kueleza kuwa zoezi hilo ni endelevu kwaajili ya kuimarisha ulinzi wa wageni na wananchi.
"Zoezi hili la ufungaji wa Kamera hizi za kisasa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa wageni pamoja na wananchi umegharimu zaidi ya milioni 200 na bado tunaendelea na zoezi hili la ufungaji wa kamera kuelekea michua mikubwa ya AFCON napia ni sehemu ya kuboresha Jiji letu la Arusha". Amesema Hamsini.
"Katika hawamu hii ya kwanza tumeamua kuweka maeneo yote muhimu ambayo kwasasa yana msongamano wa watu wengi kama kaloleni, Mianzini, Philips, Njia ya Dodoma, Sekei, Uzunguni yote na maeneo yote ya katikati ya mji kama mnavyo jua Arusha ni Jiji la Kitalii azima liwe na usalama wa kutosha kwa wageni na wenyeji". Aliongeza Hamsini.
Aidha Hamsini ameeleza kuwa Kamera hizo zimefungwa katika maeneo yote ya barabara kuu za Mjini na zile za kuelekea mikoani na sehemu zote za starehe zinazo fanya kazi masaa 24 pita kuhakikisha wqgeni wote wanaofika Arusha wawe na usalama wa kutosha.
"Toka tumeanza kufunga hizi kamera tayari tunaona zimeanza kuzaa matunda baada ya kuwakabidhi jeshi la polisi kuendelea kuzifuatia katika matukio mbali mbali ya kiharifu kitu ambacho tunajivunia ni kuona Arusha inaendelea kuwa salama maana Jiji letu linaongoza kwa kupokea wageni wengi kutoka mataifa mbali mbali kuja kutalii katika hifadhi zetu za taifa". Alisema Hamsini.
Aidha katika hata nyingie Hamsini ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Arusha inaedelea na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo kama ilivyo pendekezwa.
Post A Comment: