Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kimejipanga kuendelea kufanya utekelezaji wa mradi wa (HEET)unaofanyika sambamba na Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 25, kwa kushirikisha wadau kutoka sekta ya umma na binafsi katika kuimarisha uchumi wa viwanda ilikuendana na uchumi wa kati na kuongeza fursa za ajira kwa makundi mbalimbali hususani vijana kwa kuandaa mitaala itakayotoa wataalam wanaoendana na soko la ajira.

Ili kufufua na kupanua uwezo wa vyuo vikuu na kuchangia katika maeneo muhimu ya uvumbuzi, maendeleo ya kiuchumi, na umuhimu wa soko la ajira, kwa kuwekeza katika miundombinu inayohitajika kwa ufundishaji na utafiti wa kisasa na mzuri, na kwa mafunzo ya kiwango cha juu zaidi walimu, watafiti na wasimamizi wanaohitajika ili kufikia uwezo wao kamili.

Hayo yamesemwa na Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Prof. Epaphra Manamba, wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri wa Kitasnia (Industrial Advisory Committee) katika Kampasi ya Arusha, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

Prof. Manamba amesema kamati hii inayoundwa na wataalam wabobevu katika fani tofauti kutoka sekta ya Umma na binafsi, itasaidia katika kushauri Chuo kuhusu uandaaji wa mitaala inayoendana na mahitaji ya soko, mahitaji ya jamii na namna sahihi ya kuwafundisha wanafunzi.

" Kamati hii itapitia mitaala yetu kuona ipi inahitaji maboresho, kipi cha kuongeza, lengo likiwa ni kuhakikisha wahitimu wataotoka IAA wanakuwa na uwezo wa kuajiriwa, kujiajiri wenyewe, kujinufaisha wenyewe na kunufaisha jamii na Taifa kupitia elimu watakayopata," amesema Prof. Manamba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Kisekta IAA Bw. Joramu Nkumbi amesema kazi kubwa ya kamati hii ni kushauri namna ya kuziba ombwe lililopo kwenye soko la ajira la baadhi ya wanafunzi kushindwa kufanyia kazi kile walichofundishwa chuoni pale wanapoenda sokoni (ajira).

Ameongeza kuwa pia kamati hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kuishauri IAA kuongeza mapato kwa zaidi ya asimilia 20 nje ya makusanyo ya Ada kupitia taaluma, tafiti na ushauri wa kitaalam.

Naye mratibu wa masuala ya uhusiano wa kitasnia ( industrial linkage) Bi. Lorna Mwijarubi amesema kupitia uwepo wa kamati hiyo IAA inatarajia kutoa wahitimu wabunifu katika maeneo ya kazi za kujiajiri na kuajiwa ambao wataendana na mahitaji ya wakati ya soko la ajira kwenye sekta ya Umma na binafsi pia.







Share To:

Post A Comment: