KATIKA hali ya kushangaza Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, Juma Chikoka anadaiwa kukataa kupokea misaada ya maendeleo wilayani kwake kwa kile kinachoelezwa kuwa mtifuano wa kisiasa huku mwenyewe akikanusha madai hayo.
Hatua hiyo inatokana kukataliwa misaada hiyo inatokana na hofu ya hali ya kisiasa huku ikidaiwa kuwa wadau hao wa maendeleo huenda wana nia ya kuwania jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo kwa sasa Jimbo la Rorya linaongozwa na Mbunge Jaffari Chege.
Wadau hao wa maendeleo jana walianza kazi ya kukabdhi misaada hiyo katika maeneo mbalimbali Wilayani Rorya ambapo misaada imepatikana kwa kushirikiana na marafiki zao wamekuwa na zoezi ya kugawa madawati 20 kwa kila shule kwenye shule zote za msingi 132 zilizopo Wilayani Roya kama hatua kumuunga mkoano Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Katika kile kinachoelezwa hofu ya kisiasa DC Chikoka, aadaiwa kugoma kutokabidhiwa kwa madawati hayo zaidi ya 800 kwenye zote hizo jambo ambalo limezua sintofahamu wilayani hapa.
Wadau hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa zamani ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Rorya, Sango Kasera, ambaye kwa sasa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, waliendesha harambee kwa kushirikana na wadau wengine walipo maeneo mbalimbali nchini ambapo wamefanikiwa kupata madawati pamoja na vitanda 60 kwa ajili ya kusaidia zahanati na vituo vya hapa wilayani Rorya.
Akizungumzia hali hiyo Diwani wa Kata ya Komuge, William Nestory Marwa alisema kuwa katika hali ya kushangaza jana alipewa taarifa na mtendaji wake wa kata ambaye aliitisha viongozi wote wa ngazi ya kata na kutoa maagizo ya kutopokelewa kwa misaada hiyo.
“Wajumbe wa kamati ya siasa pia amewaambia kuwa amepewa onyo na DC kutopokea misaada hii, lakini naye nikamwambia basi mwambie Malengu (Katibu kata wa CCM) aje kupokea naye akaniambiaamepewa onyo hakuna viongozi wa CCM kuingia...
“Hivi mimi nimebaki hoi ninauliza shida ni nini Malengo amesema ameambiwa amepewa hela na wewe (Sango) ya kufanya sherehe yake ya kubariki ndoa, nikaema mimi siwezi kuacha kuja naye mtendaji wangu wa kata ananiamba hawezi kukanyaga (kuja) sasa nauliza kuna shida gani, ameniambia DC amesema yeye amepokea madawati na amazindua na hakuna mtu mwingine wa kuja kufaya hivyo.
“Hata mratibu wa elimu niamwambia nenda pale kwa kuwa hao wadau wamefika naye ananiambia nimetoka kidogo, nikabaki namuuliza sasa tunafanyaje. Kwani wanawaza nini kwani unagombea ubunge kwa kupiga kampeni?,” amesema na kuhoji
Diwani huyo amesema kuwa anashangazwa kuwa onyo hilo la kutopokea madawati hayo linatokana na nini.
“Ninawashukuru nyinyi kama waau wa maendeleo katika Wilaya yetu ya Rorya na kwa hakika madawati yamefika na mmeniokoa na adha waliyokuwa wanaipata wanafunzi katika shule za kata yanu,” amesema.
Pamoja na hali hiyo Wilaya ya Rorya pia imebainika kuwa na uhaba wa matundu vya vyoo katika shule zake huku baadhi ya majengo hayo ya vyoo yakilazimika kufungwa kutokana na kuchakaa na kuhatarisha usalama wa wanafunzi.
KAULI YA DC
Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka, alisema kuwa wialaya yake bado inahitaji kupata misaada ya wadau ili kuweza kusukuma maendeleo katika jimo hilo na hajawahi kuzuia misaada ya wadau DC Chikoka, alisema kuwa Mkoa wa Mara uliweka utaratibu wa kupokea misaada katika ngazi mbalimbali ikiwamo katika wilaya
Ambapo wadau hutakiwa kuandika barua ya nia yao au hata kuombwa na hupokelewa na ofisi yake kisha naye hukabidhi kwa Mkurugenzi ili kuipeleka kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi.
“Kwanza nikushukuru siwezi kuzuia misaada na haitokea kufanya hivyo, ila hao wanaotoa misaada wapo ambao wana nia ya kutaka ubunge utaratibu wetu ni kwamba tayari hapa yupo Mbunge (Jaffari Chege) anatakiwa kupewa ushirikiano.
“Na leo ukiruhusu kila ambaye ana msaada wake kwa kipindi hiki apite kwenye maeneo ya kata na vijiji si itakuwa vurugu, hawa wapeleke madawati ambayo tayari nimeshayapokea lakini wao walitaka tena waanze kupelekea.
" Utaratibu ukishapokea misaada hasa kama mimi DC ninatakiwa kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye yeye anajua zaidi ni eneo gani lenye mahitaji kwa wakati huu,” alisema DC Chikoka
Post A Comment: