Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent L. Bashungwa ameungana na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - KKKT Usharika wa Omurushaka, Dayosisi ya Karagwe Katika Ibada ya Jumatatu ya Pasaka.
Ibada hiyo imeongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, leo tarehe 01 April 2024.
Akitoa Salamu, Waziri Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania ya kufanya shughuli uzalishaji mali na kuleta ustawi.
Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Serikali iendelea kutekeleza miradi mbalimbali na kuboresha huduma za kijamik ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa barabara ya Nyakahanga - Nyaishozi kuelekea Benaco kwa Kiwango cha lami.
“Serikali inaendelea na Ujenzi wa barabara kwa Kiwango cha lami ya Nyakahanga kuelekea Benaco, Barabara ya kuanzia Kyerwa - Nkwenda hadi Omurushaka tumeshasaini na Mkandarasi pia tupo tunamtafuta Mkandarasi wa kujenga barabara ya Omugakorongo Mpaka Murongo” amesma Bashungwa.
Kadhalika, Bashungwa amemshukuru Askofu Dkt. Benson Bagonza kwa kuendelea kuishauri vema Serikali katika masuala ambayo wananchi wamekuwa wakiyahitaji na yanayohusu jamii na Watanzania.
Kwa upande wake, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza ameishukuru Serikali kwa kutimiza ahadi na kukamilisha Ujenzi wa barabara inayoanzia kibao cha Rukajange hadi Kanisa kuu la Dayosisi kwa kiwango cha lami.
Askofu Bagonza amiomba Serikali kuangalia kwa ukaribu suala la uwepo wa vizuizi (barrier) vingi vya kukusanya ushuru ambapo ameeleza zinaendeleza umasikini kwa Wananchi wa wilaya Karagwe.
Post A Comment: