KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeipongeza Wizara ya Maji kwa utekelezaji wa mradi wa maji wa Itagutwa ambao unahudumiwa jumla ya wananchi 1645 wa Kijiji cha Itagutwa.


Pongezi hizo zimetolewa l Mkoani Iringa baada ya Kamati hiyo kutembelea mradi, ambapo imejionea kazi zilizofanyika zikiwemo za ulazaji mabomba wa umbali wa kilometa 12.75 , Ujenzi wa vituo 11 vya kuchotea maji pamoja na ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita elf 75.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) amesema utekelezaji wa mardi huo, utasaidia kutatua changamoto ya maji kwenye Kijiji cha Itagutwa pamoja na baadhi ya vitongoji vilivyopo kwenye vijiji vya Jirani.

Akiwasilisha taarifa ya Mradi Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Iringa Mhandisi Exaud Humbo ameelezea kuwa kuwepo kwa mradi huo kutaongeza shughuli za uzalishaji kwa kuokoa muda wa wananchi waliokuwa wakiutumia kutafuta maji.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maji, Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Wizara inaendelea na jitihada ili kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi wote.

Kadhalika Mahundi amemuagiza Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Iringa Mhandisi Exaud Humbo kuhakikisha anasimamia vijiji vya kipengele na Mapululu viweze kujengewa vituo sita vya kuchotea maji, huku vijiji viwili ikiwemo Kijiji cha Kipengele vijengewe vituo vitatu vya kuchotea maji na mpaka kufikia tarehe 30 Aprili, 2024 viwe vimekamilika.

Ikumbukwe kuwa mradi wa maji wa Itagutwa ulisainiwa tarehe tarehe 16 Januari 2023 na utekelezaji wake ulianza tarehe Mei 10 2023 na gharama ya mradi huo ni shilingi milioni 322.



Share To:

Post A Comment: