Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso(MB) amewasili jijini Arusha kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama ikiwa ni siku moja tu baada ya maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi kutoka kwa Katibu wa NEC Itikati, Uenezi na Mafunzo CCM Ndg.Paul Makonda.
Akiwa jijini Arusha ameianza kazi kwa kufanya vikao vya ndani na Serikali ya Mkoa na Wilaya ya Arusha pamoja na kuketi na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Arusha.
Katika hatua nyingine Waziri Aweso amefanya ziara ya aina yake kwa kushtukiza katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Arusha kujionea hali halisi ya utoaji huduma na upatikanaji wa maji na kupata fursa ya kuwasikiliza wananchi.
Aidha, Akizungumza baada ya kuzungukia mitaa mbalimbali Aweso amekemea vikali changamoto zilizobainika na kutoa siku 30 kwa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Arusha (AUWSA) kuhakikisha wanaboresha matatizo yote.
Changamoyo zilizoonekana kwa haraka ni pamoja na maunganisho mapya ya huduma ya maji kwa wateja eneo lenye malalamiko kwa muda mrefu, Huduma kwa wateja isioridhisha, upotevu wa maji na mambo mengine.
Waziri Aweso kwa hisia akizungumza kwa hisia kali, amesisitiza suala la ushirikishwaji wa wananchi katika kupata taarifa na kutowabambikia bili za maji na kutanabaisha kuwa ni muda muafaka sasa wa Serikali kuanza matumizi ya Mita za Lipa kabla (Pre-paid meter).
Akihitimisha amemtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Arusha AUWSA Mhandisi Rujomba kufanya mabadiliko ya vitengo mbalimbali na kuondoa watu wazembe ikiwa ni pamoja na kutengeneza mpango kazi mpya.
Post A Comment: