Wakuu wa Idara/Vitengo pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) wanashiriki mafunzo ya Mfumo mpya wa kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (_National e-Procurement System of Tanzania – NeST_) ambao ni mbadala wa mfumo wa awali wa Tanzania National e Procurement System yaani (TANePS).
Dkt. Janemary Ntalwila akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu TAWIRI, ametoa wito kwa watumishi hao kuzingatia mafunzo hayo yenye tija katika manunuzi ya umma “zingatieni mafunzo na kufanya majaribio zaidi “amehimiza Dkt. Ntalwila
Bw. Japhet Laizer ambaye ni miongoni mwa wakufunzi wa mafunzo hayo, amesema mfumo wa NeST ni Mfumo mpya wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma umelenga kutatua changamoto za mfumo wa awali wa Taneps .
Aidha, Laizer ameeleza NeST ni mfumo bora na salama kwani umetengenezwa na Watanzania, pia ni mfumo rafiki na rahisi kwa watumishi ambao utasaidia kudhibiti rasilimali za Serikali na utazuia mianya yote ya upendeleo na rushwa katika mchakato wa manunuzi, kuharakisha utendaji na kuongeza uwazi.
Mafunzo haya ya siku tano yanafanyika kwa nadharia na vitendo katika Makao Makuu ya TAWIRI, Njiro – Arusha.
Post A Comment: