Watendaji wa Kata,Mitaa na Vijiji Wilayani Geita, wametakiwa kuhakikisha wanatenda haki na kujiepusha na vitendo vya rushwa Wakati wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya Urai(NIDA)
Akizungumza katika kikao cha maelekezo ya ugawaji wa vitambulisho hivyo kwenye Halmashauri ya Mji wa Geita , Mkuu wa Wilaya ya Geita Cornel Magembe amewataka Watendaji wa Kata na Mitaa kuwa wabunifu wakati wa zoezi.
“Niwaombe sana Watendaji kuzungatia sheria ambazo zimewekwa vitambulisho vinatolewa Bure nitashangaa kusikia kama kuna mtendaji anawatoza fedha wananchi wetu tunataka kila Mwananchi apewe kitambulisho kwani ni bure na ni haki yake kukipata”Cornel Magembe Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Naye Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Geita Emmanuel Ernest amesema ifikapo machi 30 mwaka huu watagawa vitambulisho zaidi ya laki sita.
Wilaya ya Geita imeandikisha watu zaidi ya laki nne vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambapo zoezi la kuvigawa limenza kufanyika na wananchi wamehimizwa kujitokeza kwenda kuchukua vitambulisho hivyo katika ofisi za serikali za mitaa kata.
Post A Comment: