WASHINDI Wa promosheni ya Twenzetu Ivory Coast Ki-VIP wawili waagwa rasmi katika Uwanja wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kuelekea Abidjan nchini Ivory Coast kushuhudia Michuano ya Afcon.
Akizungumza na Wanahabari Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Juvenalius Rugambwa amesema kupitia droo ya promosheni ya Twenzetu Ivory Coast Ki-VIP na Tigo ambapo kwa kushirikiana na tigopesa iliwapa wateja wa kubashiri na betika kwa kutumia Tigopesa na kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo TV inch 42 pamoja na king’amuzi cha dstv pamoja na Tiketi ya kushuhudia Michuano ya Afcon Abidjan nchini Ivory Coast Ki-VIP.
“Tunawasindikiza mabingwa wawili wa awali hivyo nikiwa kama Afisa Habari nitasafiri nao na tumewagawanya katika makundi mawili ambapo kundi hili la kwanza litakwenda kushuhudia mchezo kati ya Taifa stars pamoja na Morocco na Kundi la pili litashuhudia mechi kati ya Taifa stars na Mozambique utakaochezwa January 20,2024 Abidjan nchini Ivory Coast ambapo jumla ya washindi 06 wamepatikana katika droo hiyo ambapo wamegharamiwa kila kitu. “
Hata hivyo Rugambwa amesema Betika imesimamia na itaendelea kuhakikisha washindi hao na wengine watashuhudia Michuano hiyo mubashara na kupata huduma zenye hadhi (VIP).
“Kuna baadhi ya washindi tulipata changamoto kwa upande wa passport hivyo sisi kama Betika ikishirikiana na tigopesa tumelishughulikia kuhakikisha wanasafiri kuona Michuano hiyo na kuona timu ya Taifa stars na kuwapa hamasa zaidi dimbani “
Kwa upande wake miongoni mwa washindi wa promosheni hiyo waliojishindia tiketi ya kushuhudia Michuano hiyo Naseeb Stanford amewaomba watanzania kuiomba timu ya Taifa stars kufanya vizuri Michuano hiyo huku akiweka wazi kuwa wao wataenda kuipa sapoti timu hiyo dimbani.
Post A Comment: