WANAWAKE wa mkoa wa Lindi wametakiwa kuchangamkia fursa zinazopatikana sekta ya madini ambazo zinaweza kuwainua kiuchumi na kuwapa maendeleo.
Akiongea katika ufunguzi wa semina ya matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wachimbaji Tanzania na Mwenyekiti wa wanawake (UWT) mkoa wa Lindi Palina Ninje amewataka wanawake wa mkoa wa lindi kuchangamkia fursa zinazojitokeza hasa kwenye sekta ya uchimbaji wa madini kwa sekta hiyo.
Ninje alisema kuwa kwenye sekta ya madini wamekuwa wanaipa kisogo wakati ndio kuna fursa nyingi za kiuchumi na kusema kubwa sekta ya madini imeonekana kuwa na idadi ndogo ya wanawake hivyo wanawake wa Lindi wachangamkie fursa hizo.
"Niwaombe saana wanawake wenzangu kuacha kukaa vibarazani na kupiga umbea, badala yake wajitokeze kwenye utafutaji kwani kwa miaka hii ya sasa hakuna mwanaume anayeweza kumpenda mwanamke asiyejua kutafuta pesa na kuzitumia akili zake katika kusababisha maendeleo kwenye familia" alisema Palina.
Katika Hafla hiyo ya uzinduzi wa semina ya utumiaji wa nishati safi na salama ya kupikia palina Ninje amekabidhi majiko majiko ya Gas yenye thamani ya Tsh.6,750,000 kwa wanawake 150 kutoka katika wilaya tatu za mkoa wa lindi ikiwa wilaya hizo ni Ruangwa, Liwale na Lindi vijijini.
"Sisi umoja wa wanawake wachimbaji Tanzania(TWIMMI) Lengo letu na mikakati yetu ni kuhakikisha tunaisaidia serikali yetu pamoja na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwafikia wanawake wote wajasirimali kwenye nchi yetu na kuwapa elimu ya matumizizi ya nishati safi na salama itakayozilinda afya zao ili kutengeneza familia zenye wamama bora.
Kwa upande wake Meneja wa biashara wa benki ya CRDB mkoa wa lindi Godfrey Mbeshi amesema kupitia programu ya IMBEJU inawahakikishia wanawake wajasiriamali na wanawake wachimbaji wanaofahamika kwa utambulisho wa Taasisi ya Umoja wa wanawake wachimbaji Tanzania( TWIMMI), CRDB bank iko tayari kuwapatia mitaji pindi tu inapojiridhisha kuwa wanawake hao wapo katika vikundi vinavyotambulika kisheria.
Naye Micky meneja masoko STAMICO amewataka wanawake wajasiriamali kuachana na matumizi ya nishati hatarishi ya kuni na mkaa usio rafiki kwa afya na badala yake watumie mkaa salama unaotokana na makaa ya mawe.
Micky alisema mkaa wenye gharama nafuu na usio na madhara kwa afya zao ambao unazalishwa na STAMICO (Rafiki Briquettes) ikiwa pia unasaidia kwa asilimia kubwa kujilinda na magonjwa na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na vizazi imara endelevu.
Post A Comment: