Sikitu Sikitu Mwalusamba Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya Nachingwea akiongea na waandishi wa habari malengo ya wiki ya sheria wilaya ya Nachingwea 



Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

UONGOZI wa mahakama wilaya ya Nachingwea imewaomba wananchi kujitokeza katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa na mahakama kupata elimu ya sheria ili kuweza kupata namna bora ya kupata haki yao endapo watakuwa na mgogoro wa kisheria.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria wilaya ya Nachingwea yenye kauli mbiu inayosema “Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa:Nafasi ya mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai” Sikitu Sikitu Mwalusamba Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya Nachingwea alisema kuwa wamekuwa wanatoa elimu ya sheria kila wakati hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kupata elimu hiyo kila inapotokea.


Mwalusamba alisema kuwa lengo la kutoa elimu ya sheria katika wilaya ya Nachingwea ni kuwasaidia wananchi kuzijua haki zao za msingi ili wasidhurumie haki pale inapotokea Kuna mgogoro wa kisheria.


Alisema katika wiki hii ya sheria wamejipanga kwenda kutoa elimu ya sheria katika soko kuu la wilaya ya Nachingwea,shule ya wasichana wa Nachingwea na Kilimarondo lakini kutakuwa na shughuli mbalimbali ambazo zitafanyika katika wiki hii ya sheria wilaya ya Nachingwea.


Awali katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea Haji Mubaruk Balozi aliiomba mahakama ya wilaya hiyo kendelea kutoa elimu ya sheria kwa kuwa bado kunachangamoto kubwa ya wananchi wa Nachingwea kutojua vizuri sheria mbalimbali za nchi 


Balozi alisema kuwa serikali imekuwa ikibadilisha mara kwa mara na kuziboresha sheria hivyo ni muhimu kila wakati kuwakumbusha na kuwapa elimu wananchi wa Nachingwea.

Share To:

Post A Comment: