WANANCHI wa wilaya ya Nachingwea wameongeza Mahakama ya wilaya ya Nachingwea kwa kutoa elimu ya sheria bure jambo ambalo linasaidia kuzijua haki za kila mwananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria wilaya ya Nachingwea, Frank Mohamed ambaye ni mwananchi wa Kijiji cha Nang’olola alisema kuwa amefanikiwa kupata elimu ya sheria kutoka kwa mmoja wa maafisa kutoka ofisi za mahakama namna gani ya kupata haki ya mali alizokuwa amedhurumiwa.
Mohamed alisema kuwa alidhurumia shamba kwa kutokujua namna gani anaweza kupata haki yake hivyo baada ya kupata elimu ya sheria anaenda kufungua kesi ili aweze kupata haki ya kumiliki shamba alilokuwa amedhurumiwa.
Aisha abdalah mkazi wa Matangini alisema kuwa amefurahi kupata elimu ya sheria ambayo itamsaidia kwenda kudai taraka kwa aliyekuwa mme wake ambaye amekuwa hataki kutoa taraka kwa hiyari
Abdalah alisema kuwa amepata elimu hiyo wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria wilaya ya Nachingwea katika uwanja wa Saba Saba wakati mchezo wa mpira miguu ukiwa unaendelea kutoka afisa mmoja kutoka Mahakama ya wilaya ya Nachingwea.
Nao baadhi ya wananchi walisema kuwa uongozi wa Mahakama wilaya ya Nachingwea wanajitahidi kutoa elimu ya sheria na kuwaomba pia kuwafikia wananchi walioko vijijini ili wajue haki zao.
Walisema kuwa wananchi wengi walioko vijijini wanapoze haki zao kutokana na kutokujua sheria ambayo ingemsaidia kutafuta haki yake
Post A Comment: