HOSPITALI ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma kupitia Kitengo cha Kifua Kikuu na Ukoma ,imeanza kampeni maalum ya upimaji wa vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu kwa wanafunzi wa shule zote za msingi na sekondari wilayani humo.
Mratibu wa kitengo cha kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Tunduru Dr. Mkasange Kihongole amesema wanafunzi wa bweni watakaokutwa na maambukizi ya TB wataanzishia dawa kama mkakati wa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo katika wilaya ya Tunduru
Akizungumza katika kampeni ya uelimishaji,uibuaji na uchunguzi wa ugonjwa huo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Kiuma.
“Tunaamini kuwa tunapotoa elimu ya kifua kikuu kwa watoto hasa wanafunzi ni rahisi sana ujumbe kuwafikia watu wengi katika jamii ambao hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na ugonjwa wa TB”,alisisitiza
Amesema ,watoto wanapokuwa likizo wanakuwa kwenye muingiliano na watu mbalimbali na miongoni mwao wapo wanaougua kifua kikuu,hivyo wao kuwa katika hatari ya kupata maambukizi bila kujitambua,na kwamba wanaporudi shuleni ni rahisi kuambukiza wengine.
Amesema kampeni hiyo inafanywa na ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya kupitia Kitengo cha Kifua kikuu na ukoma kwa kushirikiana na Idara ya Elimu ya Msingi na Sekondari .
Amesema kuwa,katika kampeni hiyo wanafunzi watakaobainika kuwa na maambukizi ya kifua kikuu watapata matibabu mapema ili wasiambukize wengine .
Serikali imedhamiria kutokomeza ugonjwa ugonjwa wa kifua kikuu ifikapo mwaka 2030.
Post A Comment: