Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni, akifungua kikao cha wadau na wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mtwara Machi 22, 2024.
...........................
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
WADAU wa Afya wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mtwara
wamehimizwa kusimamia matumizi sahihi ya takwimu za mnyororo wa ugavi wa bidhaa
za afya, ili ziwawezeshe kufanya maamuzi sahihi juu ya bidhaa hizo katika
maeneo yao.
Akifungua kikao cha wadau na wateja wa MSD kanda
ya Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni amesema uwepo wa takwimu
sahihi unaiwezesha MSD kuagiza kwa usahihi bidhaa za afya na kuboresha
upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Aidha, amewashauri MSD kuhakikisha utaratibu wa
vikao vya mwaka vya wadau ni muhimu kwa
pande zote mbili, yaani Bohari ya Dawa (MSD) yenyewe na wadau ili kwa pamoja
kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya, kwa kujadili changamoto na kuzitafutia
utatuzi.
Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Mtwara Tea Malay
ameeleza kuwa kwa sasa kanda ya MSD Mtwara inahudumia vituo vya kutolea huduma
za afya 631, na inasambaza bidhaa za afya kila baada miezi miwili.
Naye Meneja Huduma kwa Wateja na Miradi Dkt.
Pamella Sawa ameeleza kuwa vikao vya MSD na wadau wake kuanzia sasa vitakuwa
endelevu kila mwaka.
MSD Kanda ya Mtwara inahudumia mikoa ya Lindi,Mtwara na Wilaya ya Tunduru.Meneja wa MSD Kanda ya Mtwara Tea Malay, akizungumza kwenye kikao hicho
Post A Comment: