Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Chatanda kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali wametoa mafunzo maaalum kwa viongozi wanawake kutoka mikoa 9 ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Ziwa Magharibi. Dhima kuu ikiwa ni kuwajengea uwezo Wanawake namna ya kutumia matokeo ya Sensa katika kuchochea maendeleo sanjari na Kuleta ufanisi wa Utendaji wa kazi katika kujikwamua kiuchumi na kijamii.
Mafunzo hayo ya Siku moja yamehusisha viongozi wanawake pamoja na Waheshimiwa Madiwani Viti Maalum kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Katavi, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kigoma, Tabora pamoja na Mkoa wa Mara leo tarehe 27/3/2024 Katika Ukumbi wa Winterfell Mkoani Mwanza.
Kadharika mafunzo hayo yamehudhuriwa na Mhe. Anne Makinda Spika Mstaafu wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamisaa wa Sensa, Katibu Mkuu wa UWT Ndg. Jokate Mwegelo, Naibu katibu Mkuu UWT Bara Ndg. Riziki Kingwande pamoja na Mhe. Amina Makilagi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Post A Comment: