Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa lindi Palina Ninje amewapatia mitungi ya Gas ya kupikia yenye thamani ya Tsh. 2,250,000/= wanawake wajasiriamali 50 wanaojishughulisha na upikaji wa mama lishe katika kijiji cha somanga, kata ya somanga, wilaya ya kilwa Mkoani lindi.
Akizungumza na wanawake hao palina amesema ametekeleza hayo ili kuunga jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu hassan anazopambana nazo kuhakikisha wanawake wanaondokana na utumiaji wa nishati isiyo salama kwa maisha yao na badala yake watumie nishati salama.
“Rais wetu ametuonyesha jinsi gani anahitaji akina mama na wananchi wa Tanzania kwa ujumla wanatakiwa kutumia nishati salama ili Taifa liwe na wananchi wenye afya bora na wasio na magonjwa hasa kifua kikuu, matatizo ya moyo, homa ya mapafu na magonjwa mengine yatokanayo na matumizi ya majiko yanayochafua hali ya hewa pamoja na kuzuia ukataji wa miti ovyo hali inayopelekea mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababisha maafa katika jamii zetu tunazoishi hivyo nikaona nifanye jambo hili leo katika eneo hili linaloongoza kuwa na mama lishe wengi wanaoingizia wilaya ya kilwa kipato kikubwa na kusababisha maendeleo kwa kasi” Alisema Bi palina.
Katika zoezi hilo Bi palina alipokea wanachama 50 waliojiunga na jumuiya ya wanawake UWT na kuwapatia kadi 50.
“Niwaombe saana akina mama tumuunge mkono Rais wetu kwani tunaona anavyokesha usiku na mchana kwa kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kwa kasi kubwa ya maendeleo” alisema.
Kwa upande wa wanawake wajasiriamali kijijini hapo wameishukuru serikali na Rais Samia kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake wote duniani.
Wakitoa changamoto wanazozipitia katika biashara hiyo wajasiriamali hao wameiomba serikali kufanya jitihada za haraka za kwenda kuwapatia elimu na mikopo halali ya serikali kwani wanapitia mateso na udhalilishaji kutokana na mikopo ijulikanayo kwa jina la (KAUSHA DAMU)
Kwa niaba ya wajasiriamali hao Bi mwajabu said, amesema wamekuwa wakinyang’anywa mali na vifaa vya biashara mara kwa mara na hii ni kutokana na kukosa sehemu salama ya kukopa pesa za kuongeza mitaji yao.
Post A Comment: