Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akizungumza wakati akifungua semina ya Elimu kwa Mlipakodi ilioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa viongozi wa mashirikisho ya waendesha bodaboda na Bajaji
Naibu Kamishna wa walipa kodi wadogo na kodi za ndani, Edmund Kawamala, Akizungumza wakati wa kufungua semina ya Elimu kwa Mlipakodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa viongozi wa mashirikisho ya waendesha bodaboda na bajaji nchini. Semina hiyo imefanyika leo Machi 24, 2024 katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam.

SERIKALI imesema itaendelea kujenga mahusiano mazuri na waendesha bajaji na pikipiki maarufu kama bodaboda pamoja na kushiriana nao kwani kazi hiyo ni kama kazi zingine na eneo hilo linaloongeza pato la taifa katika ukusanyaji kodi.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema hayo leo, Machi 25, 2024 wakati akifungua semina ya Elimu kwa Mlipakodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa viongozi wa mashirikisho ya waendesha bodaboda n Bajaji kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

"Serikali inatambua bodaboda na bajaji kama ajira zingine na hakuna utofauti na viongozi wengine hivyo tuheshimu kazi zao na baada ya elimu hii tuendelee na  umoja wetu, na nawaomba ninyi viongozi mliofika hapa leo mkishapata elimu hii basi mkawe mabalozi kwa wengine pia" amesema Mpogolo

“Niwapongeze TRA kwa kuandaa mkutano na watu hawa kwani ni imani yangu baada ya kuwapatia elimu hii kwa mlipakodi tutaendelea kujenga ushirikiano mzuri

Aidha, amemshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu bodaboda na bajaji kufika katika ya mji kwani ndio walipa kodi…,zaidi ya Shilingi Milioni 27 zimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha bodaboda na bajaji kukopa na kufanya shughuli zao za Kila siku na leo hii TRA wamewatambua zaidi kwa kuwapa elimu ya kulipa kodi ili kukuza uchumi wa nchi, tupate maendeleo,"  ameongeza Mpogolo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano TRA Hudson  Kamoga amewataka waendesha bodaboda na bajaji kufatilia umiliki halali wa vyombo vya moto pale wanapokuwa wamemaliza mikataba yao ili waweze kukuza pato la taifa na kuwa mfano bora katika ulipaji kodi.

"Nchi haiwezi kuendelea bila mapato kwani hata miradi inayoendelea kujengwa inatokanana na kodi za wananchi, hivyo ninyi madereva wa vyombo vya moto unampomaliza mkataba na mmiliki wa chombo kikawa chako hakikisha ubadili jina ilikupata umiliki kwani kushindwa kufanya hivyo unasababisha hasara kwa Taifa," alisema.

Ameongeza:"kukosekana kwa elimu juu ya bodaboda na bajaji kunapelekea watu hawa kukosa haki zao za msingi pale anapopata changamoto kwani kadi inasoma jina tofauti na ailie na chombo cha moto na ukifatilia unakuta kweli mmiliki ni huyu aliepata changamoto"alisema Kamoga

Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Madereva Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dar es salaam ,Said Kagomba amewashukuru TRA kwa kuwaita kwa ajili ya kuwapa elimu ya kulipa kodi kwani watu wengi tulikuwa hatulipi kodi kutokana na kutumia jina ya la mmiliki wa kwanza.

"Tunashukuru kwa kupata elimu hii kwani madereva wengi tulikuwa Bado tunatumia majina ya zamani na pia watu wengi hawana leseni jambo linalopelekea akipata ajari anakosa msaada",Kagomba alisema.

Ameongeza kuwa: "Niwaombe madereva kuzingatia taratibu zote za kulipa kodi na kuwataka wanachama wa shirikisho kwenda kutoa elimu hii kwa madereva wengine kama darasa la mabadiliko na kuachana na ukwepaji kodi kwani unadhoofisha uchumi wa nchi.

Vilevile aliiomba serikali kupitia TRA kutoa TIN namba hata kwa watu wasio na kitambulisho au namba ya nida zaidi wazingatie cheti cha kuzaliwa",aliongeza Kagomba.

Makamu Mwenyekiti wa Watu Wenye Ulemavu Mathew Kashiririka, amesema elimu hii ni nzuri hasa kwa watu wenye ulemavu kwani walikuwa wananyanyaswa na Wamiliki wa vyombo vya moto.

"Nashukuru sana TRA kuandaa mkutano huu kwani unatupa uelewa sisi watu wenye ulemavu kwani kunatofauti katika ya kulipa kodi kati ya mtu mwenye ulemavu na asiye na ulemavu lakini Leo tumepata ufumbuzi sambamba na Hilo tulikuwa tukipata manyanyaso kutoka kwa wamiliki lakini Leo tumejua haki zetu". Kashiririka

Naye, inspekta Samson Nguno Mkuu wa Dawati Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dar es salaam,amewataka madereva bodaboda na bajaji kizingatia alama na sheria zote za barabarani kwani wao wameonekana kuwa chanzo kikubwa cha ajali za makusudi, hivyo kupitia mkutano huu ukawe chachu kubwa kwao na kuleta mabadiliko kwani ukizingatia haya itasaidia kupunguza faini na kulipa kodi kwa ufanisi ikumbukwe faini zikiwanyingi hata ilipaji wa kodi utazorota.


Kaimu Mkurugenzi Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano TRA, Hudson Kamoga
Mwenyekiti wa bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, Said Kagomba  Akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kufunguliwa kwa semina ya Elimu kwa Mlipakodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa viongozi wa mashirikisho ya waendesha bodaboda na bajaji nchini. Semina hiyo imefanyika leo Machi 24, 2024 katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam.
Share To:

Post A Comment: