KILINGE Salama (Safe Space) kilichoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Chamwibua Diwani, Farida Abdallah ambaye ni Diwani wa wilaya ya Mtwara ambapo ameeleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanawake viongozi ikiwemwo kukatishwa tamaa ili wasiweze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Akizungumza leo Machi 28, 2024 wakati wa kilinge salama kilichofanyika katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam, Diwani huyo ambaye aliishia kidato cha pili na kupata ujauzito huku akimpote Mama yake mzazi amewaasa wanawake kutokukata tamaa pale yanapojitokeza maneno ya kukatisha tamaa pale yanapojitokeza wakati wa harakati za kutafuta nafasi za uongozi.
“Wakati nawania nafasi ya uongozi watu walikuja kunikatisha tamaa ili ni sigombee….. hata kwenda kumshawishi Mme wangu ili anikatishe tamaa lakini hawakufanikiwa….” Amesema Farida.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi akizungumza wakati wa kufungua Kilinge salama ambapo ni mazingira ambayo ni rasmi au yasiyo rasmi ambayo wanawake na wasichana wanapata nafasi ya kujadili kwa uhuru masuala yao, amesema kuwa Katika mwezi Machi wa wanawake, TGNP imekuwa ikiandaa vilinge hivyo ili kuhamasisha wanawake kuingia katika nafasi za uongozi.
“Mategemeo yangu ni kwamba mwisho wa siku ya leo tutaungana kwa pamoja kuendelea kusimamia Agenda ya mwanamke na uongozi katika mkoa wetu wa Dar es Salaam.”
Pia Mkurugenzi Mtendaji Lilian ameweka bayana takwimu za Wenyeviti wa vijiji kuwa ni asilimia 2.1, Wenyeviti vitongoji ni asilimia 6.7 na Wenyeviti mitaa ni asilimia 12.6.
Kwa upande wa Wabunge wa kuchaguliwa, wanawake ni 25 ya Wabunge 264 ambayo ni sawa na asilimia 9.5 tu ya Wabunge wote, idadi ya Wabunge wanawake wa Viti Maalumu ni 113 ambayo ni sawa na asilimia 29 ya Wabunge wote. Jumla ya Wabunge Wanawake ni 142 sawa na asilimia 37 ya idadi ya Wabunge wote ambao ni 393 ambapo ili kufikia 50 kwa 50 ya uongozi wa Wanawake Viongozi lazima ifikiwe kwa kutoa elimu kwa wanawake na wasichana waweze kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Lilia pia ameeleza kuwa malengo ya Kilinge salama kwa Wasichana na Wanawake ni kukaa pamoja na viongozi wanawake wanaochipukia na viongozi wanawake wenye uzoefu, kuandika na kusambazi kestoria za safari za uongozi za wanawake viongozi mahiri ili kuonesha michango waliyonayo katika maendeleo ya nchi.
Pia kutoa hamasa kwa viongozi wanawake wanaochipukia au wanawake wanaotamani kuwa viongozi.
Kilinge Salama kwa Wanawake na Wasichana pamoja na viongozi leo ni kutoka mkoa wa Dar es Salaam, halmashauri za Ilala, Kinondoni na Temeke, Mtwara, Lindi na Pwani.
Post A Comment: