Katika Kuelekea siku ya wanawake Duniani Wakuza Mitaala wanawake kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) wametoa mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa kwa walimu wa baadhi ya shule za Jiji la Dar es Salaam leo Machi 6, 2024 kama sehemu ya kuadhimisha siku hiyo itayofanyika Machi 8, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa TET,Dkt.Aneth Komba amesema kuwa wameamua kurudisha kwa jamii ili waweze kufadika na utaalamu wa watumishi hasa wanawake wanaosherehekea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia.

“Sisi tumeamua kuanza kusherehekea mapema kujitoa kuwapa walimu mafunzo ambayo tuna amini yatawasiaidia katika kazi zao”amesema Dkt.Komba

Mafunzo hayo yamefanyika katika shule za msingi za Oysterbay, Olimpio, Buguruni, Kunduchi, Mivumoni, Kimwani, Chamazi, Majimatitu, Mikwambe, Kigogo, Raha Leo, Kimbiji, King’azi, Tegeta na Anazaki lengo ni kujadiliana mbinu mbalimbali za kufundishia wanafunzi kuhusu Mtaala ulioboreshwa.

Katika majadiliano hayo, walimu kutoka shule hizo walipata nafasi ya kuujua Mtaala ulioboreshwa kwa undani na kutoa mawazo mbalimbali ya namna bora ya kuboresha mbinu za ufundishaji ili Mtaala huo ulete tija kwa mwanafunzi.





Share To:

Post A Comment: