Naibu waziri wa maji Maryprisca Mahundi kushoto,mbunge wa jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma Stella Manyanya wa pili kushoto na makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya maji na mazingira Anna Lupembe kulia wakijaribu kufungu
 Diwani wa kata ya Tingi katika Halmashauri ya wilaya Nyasa mkoani Ruvuma Raynald Kimwaga, akieleza changamoto zinazowakabili wananchi wa kata hiyo mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya maji na mazingira waliotembelea mradi wa maji Malungu unaotekelezwa na Ruwasa katika kijiji cha Malungu kwa gharama ya Sh.bilioni 1.2a kiko katika moja ya vitu vya kuchotea maji katika kijiji cha Malungu wilayani Nyasa.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya akizungumza kwenye mkutano wa wananchi wa kijiji cha Malungu na wajumbe wa kamati ya Bunge ya maji na mazingira(hawapo pichani)waliotembelea mradi wa maji Malungu unaotekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)kwa gharama ya zaidi ya Sh.bilioni 1.2.

 NAIBU Waziri wa maji Maryprisca Mahundi amesema,serikali imejipanga kufikisha huduma ya maji safi na salama kwenye maeneo yote yenye changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji nchini, ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki katika shuguli zao za maendeleo.


Mahundi ametoa kauli hiyo jana,wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya maji na mazingira waliotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Malungu kata ya Tingi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Alisema,serikali inajenga miradi ya maji ili kuongeza kipato cha familia na kukuza uchumi wa nchi yetu, kwa kuwa wananchi watapata muda wa kujikita kwenye kwenye shughuli za kujitafutia kipato badala ya kwenda kutafuta maji.

Aidha aliwaeleza wananchi wa kijiji hicho kuwa,serikali imeanza kufanya usanifu wa kutambua maeneo yote yasiyokuwa na mtandao wa maji ya bomba ili yaweze kupata huduma ya maji kabla ya mwezi julai mwaka huu.

Naibu Waziri,amewapongeza watendaji wa Ruwasa mkoa wa Ruvuma,kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kutekeleza miradi kwa viwango na inayolingana na gharama halisi ya fedha zinazotolewa na serikali.

Amewakumbusha wananchi wa kijiji cha Malungu na Tingi umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji ili miradi inayotekelezwa iweze kudumu kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya maji na mazingira Jackson Kiswaga,ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi ili kutekeleza miradi ya maji katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Amewaomba wananchi wa kijiji hicho,kuinuga mkono serikali katika jitihada zake za kuleta maendeleo kwa kulinda na kutunza miradi inayoendelea kutekelezwa katika kijiji hicho.

Naye Mbunge wa Jimbo la Nyasa Stella Manyanya alisema,wilaya ya Nyasa ime imebahatika kupata miradi mingi ya maji ambayo imekamilika na mingine iko kwenye utekelezaji ikiwemo mradi wa Malungu utakaohudumia vya Malungu na Tingi.

Alisema,wakati anachukua jimbo hilo hali ya upatikanaji wa maji katika vijiji vingi haikuwa nzuri na wananchi walilazimika kutumia maji ya mito na visima ambayo hayakuwa safi na salama kwa sababu walitumia pamoja na wanyama wa porini.

Kwa mujibu wa Manyanya,serikali ya awamu ya sita imesaidia sana kupunguza changamoto yam aji na wananchi kwa sasa wanapata muda mwingi wa kushiriki na kufanya shughuli za maendeleo badala ya kujikita kwenye ulevi.

Awali meneja wa Ruwasa wilaya ya Nyasa Masoud Samila alitaja gharama za mradi ni Sh.bilioni 1,222,759,056.00 ambazo zinatoka serikali kuu na mfuko wa Taifa wa maji na wakazi zaidi ya 9,659 wa vijiji viwili vya Malungu na Tingi watanufaika na mradi huo.

Alieleza kuwa,utekeleza wa mradi wa maji Malungu haukukamilika kwa wakati kama ilivyopangwa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuchelewa kuletwa kwa mabomba,hata hivyo changamoto hiyo kwa sasa imetatuliwa na mkandarasi ameongezwa muda wa kukamilisha mradi huo.

Share To:

Post A Comment: