Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka Februari 14,204 ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki mjini Njombe kushiriki Misa Takatifu ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa Katoliki jimbo la Njombe.
Misa hiyo imeongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Njombe Eusebio Kyando.
Siku ya Jumatano ya Majivu Waumini hupakwa Majivu katika paji la uso ishara na alama ya matumaini makuu, kunyenyekea na kutambua kuwa dunia ni sehemu binadamu anapita, kukiri mapungufu ya binadamu, kukiri dhambi na kutambua huruma ya Mungu ni kubwa kuliko dhambi za binadamu.
Pia kipindi cha Kwaresima huanza Jumatano ya Majivu na hudumu kwa muda wa siku 40 kuelekea siku ya Pasaka yaani mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.
Post A Comment: