Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa amewasihi na kuwaomba watendaji wa Serikali Wilayani humo kusimamia Mradi wa Maji Unaotarajiwa kuanza hivi karibuni itakayogharimu billioni 20.3 ,wa Vijiji 13.


Hayo yanajiri baada ya Kampuni ya JANDU PLUMBER ya Jiji la Arusha kufika Jimboni hapo kwa Lengo la kujitambulisha kwa Viongozi wa Chama na Serikali Rasmi Mradi huo kuanza.


Mradi huo unafuatia Ahadi za Mbunge huyo kwenye Uchaguzi mkuu 2020, Ambapo Hayati Rais John Pombe Magufuli alilipokea ikiwa ni hitaji la Mbunge huyo ,Ambapo miaka miwili baadaye Rais wa Awamu wa sita Dkt Samia Suluhu Hassan aliridhia Mradi huo Eneo la Makuyuni , Na November 2023 Waziri wa Maji Jumaa Aweso alishuhudia utiaji saini wa Mradi huo eneo la Nanja Lepurko Monduli.


Frederick Lowassa amesema Mradi huo wa Billioni 20.3 Utahudumia Vijiji 13 Ambavyo havijawahi kupata Maji safi na Salama .

" Sasa ningeomba basi, Ningeomba kwa msisitizo Mkubwa sana Kwamba Watendaji wa Serikali wasimuangushe Rais Samia Suluhu Hassan ,wasiwaangushe wanaCCM,wasiwaangushe wanaMonduli ,  watu wa Monduli Tumeahidiwa Mradi Huu Utaisha Ndani ya miezi 24 ,Tumefurahi kwamba leo mmekuja kutambulishwa na Serikali imewapokea ,Lakini Naomba Naomba sana Watendaji wasituangushe ,Ahadi hii ni kubwa Watu wa Monduli wana kiu kubwa sana"amesema Fredrick Lowassa Mbunge.


Kwa Upande wake Meneja Ruwassa Wilayani Monduli Eng Nevvile Msaki Amesema Lengo la Mradi huo ni Vijiji 13 ambapo utakuwa pia na Matawi likiwemo la Meserani , Huku kijiji cha mtimmoja kitajengwa Booster Station itakayopeleka Maji Kijiji cha Engarooji,Losimingori na Maeneo ya jirani.


Aidha Mkurugenzi  wa Kampuni hiyo ya JANDU PLUMBERS Bwana Kamal Jandu ,Kwa pamoja wamekiri kutekeleza Mradi huo Ndani ya Miezi 24, kwa usahihi na uhakika.

Share To:

Post A Comment: