NA DENIS CHAMBI, TANGA
MAMLAKA ya vitambulisho vya Taifa ‘NIDA’ mkoa wa Tanga imezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wananchi wapatao 165, 000 ambavyo vitakuwa vipatikana kupitia ofisi za kata na vitongoji ili kurahisisha upatikanaji kwa walengwa wote.
Akizindua zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amemwagiza meneja wa NIDA wa mkoa huo kuhakikisha ifikapo january 31 , 2024 wananchi wote ambao waliomba wawe tayari wameshapata huku akiwataka wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi za wilaya pale ambapo itatokea mtu yoyote kudai pesa ili weze kupewa kitambulisho chake .
“Kwa mkoa wetu wa Tanga Mamlaka yetu ya NIDA imeweza kusajili wanannchi 1, 191, 488 sawa na asilimia 88, namba za vitambulisho zilizo zalishwa ni 9, 50 ,392 sawa na asilimia 80 ya wakazi wote wenye umri wa miaka kuanzia 18 na vitambulisho vilivyopokelewa na kusambazwa ni 7, 96, 155 sawa na asilimia 83 ya wananchi wote waliokidhi vigezo ni matumaini yangu kuwa wananchi wote kupitia wilaya zote mtajitokeza kupata vitambulisho vyenu, jambo ambalo ni la kusisitiza ni kwamba vitambulisho hivi vitagawiwa bure kama itatokea mtu yeyote atakudai fedha taarifa hizo zifike mara moja kwenye ofisi za wakuu wa wilaya na hatua kali zichukuliwe mara moja” alisisitiza Kindamba.
Meneja wa Mamlaka ya vya vitambulisho vya Taifa NIDA mkoa wa wa Tanga Kitashu Lembira alisema kuwa zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho ambalo limezinduliwa na mkuu wa mkoa leo litafanyika katika ngazi za wilaya ili kuwarahisishia na kuwawezesha wananchi wote waliokidhi kupata akipongeza juhudi za serikali kwani malalamiko ya wananchi kuhusu kukosekana kwa vitambulisho hivyo muda mrefu impshapatiwa ufumbuzi.
“Tumezindua mkoani lakini kuazia jumatatu ijayo vitambulisho vyote kuanzia ngazi za wilaya kata vijiji na vitongozi vitakuwa vimeshasambazwa na kutakuwa na majina yamebandikwa kwenye mbao za matangazo , kikubwa ni kuipongeza na kuishukutu serikali hususan kwa awamu hii ya sita kwa mkoa wa Tanga tunajivunia kwa sababu ni kipindi ambacho changamoto cha kukosekana kwa vitambulisho inakwenda kuisha na kila mwenye namba ya kitambulisho cha taifa atapata kitambulisho chake” alisema Lembira
Kama alivyotuagiza mkuu wa mkoa kuwagawia vitambulisho ananchi wote wenye namba za NIDA ifikapo January 31, 2024 wananchi wote watapata na tutashusha mpaka ngazi vya vijiji na vitongoji kikubwa tywaombe tu wananchi wawe watulivu kwa sababu tumeweka utaratibu mzuri kwa yule mwananchi ambaye atakqenda na atakosa ktambulisho chake atayoa taarifa kwa mtendaji wa kata ambaye naye atalazimika kufikisha katika ngazi ya wilaya ili kitambulisho kiweze kupatikana” aliongeza
Wakizungumza baadhi ya wananchi waliopata vitambulisho vyao wakiwemo Waziri Omari na Mwanamisi Mbwana wameishukuru na kuipongeza serikali kwani kwa kuwapatia vitambulisho hivyo kumewasaidia kupata huduma mbalimbali ikiwemo za kifedha.
“Naishukuru sana Serikali kwa kutupatia vitambulisho hivyi tulikuwa tunavisubiri kwa muda mrefu tumekuwa tukikosa baadhi ya huduma , kitambulisho cha Taifa kinahusika maeneo mengi tumekuwa tukikosa huduma”
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba (kulia) akipokea vitambulisho kutoka kwa meneja wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA ‘ Mkoa wa Tanga Kitashu Lembira mara baada ya kuzalihswa na mamlaka hiyo tayari kwaajili ya kugaiwa kwa wananchi.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akikabidhi kitambulishi cha Taifa kwa mwananchi wa jiji la Tanga Waziri Omari mara baada ya kuzindua zoezi hilo leo January 17,2024 katika ofisi yake
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akikabidhi kitambulishi cha Taifa kwa mwananchi wa jiji la Tanga Mwanahawa Mbwana mara baada ya kuzindua zoezi hilo leo January 17,2024 katika ofisi yake.
Post A Comment: