WANANCHI wametakiwa kujihadhari na taarifa za upotoshaji kuhusu utaratibu wa usajili wa watoto kupitia mpango wa ‘Toto Afya Kadi’.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anjela Mziray amesema taarifa zinazosambaa mtandaoni na kudai gharama za usajili kuwa Sh 35,780 kwa mwaka Sh 95,780 kwa miaka mitano na kutaka taarifa za mtoto zitumwe kwenye namba ya Whatsapp +255735 051419.
“NHIF haifanyi usajili na kupokea nyaraka za wanachama kupitia Whatsapp wala kupokea michango ya wanachama kupitia namba za simu,” imeeleza taarifa hiyo.
Pia, NHIF imetanabahisha kuwa viwango vya uchangiaji vilivyoanishwa ni vya upotoshaji.
“Mfuko unaendelea kuwakumbusha wananchi kwamba unaendelea kusajili watoto kwa utaratibu kujiunga na mzazi/wazazi wao kupitia Vifurushi vya bima ya afya ambapo michango hutegemea uchaguzi wa kifurushi husika na idadi ya wanaojiunga,
“kupitia usajili wa ujumla wa wanafunzi kupitia shule wanazosoma ambapo wazazi/walezi na uongozi wa shule husika huwasiliana na ofisi ya NHIF iliyo karibu kukamilisha usajili huo ambapo kila mtoto atachangiwa Sh. 50,400 kwa mwaka,” imeelezea.
Imefafanua kuwa michango ya wanachama hulipwa kupitia namba ya malipo ya Serikali (control number) inayotolewa na Mfuko baada ya kukamilisha usajili na si vinginevyo.
“Mfumo rasmi wa mawasiliano uliowekwa na Mfuko ikiwemo namba ya huduma kwa wateja 199, tovuti ya Mfuko ambayo ni www.nhif.or.tz.” Imefafanua.
Post A Comment: