Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Loy Thomas Ole Sabaya, akizungumza na wananchi wa Kata ya Pinyinyi kwenye Kijiji cha Masusu wilaya ya Ngorongoro, wakati kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Masusu.
Kamati hiyo ya Siasa Mkoa, inafanya ziara ya kawaida ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kisekta, ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020 – 2025
Hata hivyo, Mwenyekiti Sabaya, ameipongeza Serikali ya Awamu ya sita, chini ya uongozi shupavu wa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, viongozi wa jamii na serikali wa ngazi zote pamoja na watalamu wa wilaya na Mkoa, kwa usimamizi imara wa miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa kishindo wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Post A Comment: