KUFWATIA maagizo ya Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi ‘CCM” Paulo Makonda aliyoyatoa mkoani Tanga akiwa kwenye ziara yake hivi karibuni kuhusu kutokukamilika kwa ujenzi wa Zahanati ya Madanga kwa muda mrefu mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman amechangia kiasi cha shilingi milioni 10 ili kuunga mkono jiyihada ambazo zilianzishwa na wananchi.
Mchango huo aliutoa january 24 mara baada ya kufanya ziara na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya ya Pangani ambapo awali Zahanati hiyo ilikuwa ikitumika lakini serikali ikasimamisha utolewaji wa huduma za afya.
Kusimamishwa kutoa huduma katika Zahanati hiyo ni kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya jengo lilolokuwa likitumika ambapo iliwalazimu wananchi kwenda mpaka Bushiri na Boza kufuata huduma hali hiyo ikapelekea wakazi wa maeneo hayo kutumia nguvu kazi zao kuanza ujenzi huo wakichangishana fedha ambazo ziliishia kwenye msingi ambao bafo haujamalizika.
Aidha wananchi hao waliendelea kujitoa kuhakikisha kuwa kiu yao ya kuona Zahanati hiyo inakamilika wakachangishana na kununua mifuko mingine 10 ya saruji ambayo haikutumika na haijulikani ilipo mpaka sasa.
Katika kuunga mkono juhudi hizo za wananchi Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa maji Jumaa Aweso alichangia mifuko 100 ya saruji pamoja tofali 300 ambavyo hata hivyo havikutumika na hivyo jengo hilo kuendelea kusua sua hadi sasa na mifuko hiyo haijulikani ilipo.
Ili kuhakikisha Zahanati hiyo inakamilika na kuwaondolea adha wananchi ya kutembea ubali mrefu wa kufuata huduma mwenyekiti wa huyo amekabidhi kiasi cha shilingi Milion 10 kwa mkuu wa wilaya hiyo Zainab Abdallah huku akitoa tahadhari kwa yeyote mwenye nia ovu ya kutaka kutumia pesa hizo kinyume na malengo akiwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto zilizopo.
“Mimi ninawaunga mkono kwa kichangia shilingi Milion 10 sasa hivi kwa ambaye hajawahi kuona rangi yangu achezee hizi fedha ninazozitoa mimi wananchi mnapolalamika sisi kama viongozi mioyo yetu inaumia , sisi kama viongozi tuna wajibu wa kuwayumikia wananchi pamoja na kutayua changamoto zinazowakabili hatujaomba nafasi hizi bure bure, panapohitajika nguvu zetu tutumieni nguvu zetu kuiunga mkono serikali kwa sababu adha hii tukumbuke ni sisi inaotukumba” alisema mwenyekiti huyo.
Viongozi wengine waliungana na mwenyekiti kichangia ujenzi huo ambapo akiwemo mkuu wa wilaya hiyo Zainab Abdallah ameahidi kutoa shilingi Milion 3, katibu wa hamasa wilaya hiyo akiahidi kutoa lori 3 za mawe, mjumbe wa kamayi ya siasa ngazi ya Mkoa Nassoro Makau akiahidi kuchangia ahilingi laki tano
Akiwa katika kata ya Mikinguni mwenyekiti huyo amechukizwa kuona ujenzi wa ofisi ya chama ngazi ya kata hiyo haujakamilika licha ya michango mbalimbali ikiwemo Milion 1 iliyotolewa na mbunge wa jimbo hilo Jumaa Aweso ikamlazimu kutoa maagizo kwa mkoa mzima kuahkikisha zinajenga ofisi zao na sii kutumia majengo ya serikali kwaajili ya kuendeshea shughuli zao ikiwemo vikao.
“Hainiingii akilini ndani ya miaka 47 tangu kuzaliwa Chama chetu cha Mapinduzi ‘CCM’ chama haikina ofisi za kata haiwezekani tukihitaji vikao vyetu tukafanye kwenye shule za Msingi sio sawa kisa tu chama ndio kina serikali wajibu wetu tujenge majengo yetu sisi wenyewe na hatushindwi” alisema.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman akikabidhi kiasi cha shilingi Milion 10 kwa kuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah fedha ambazo amechangia kwaajili ya ujenzi wa Zahanati ya Madanga iliyopo wilayani Pangani.
Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah akizungumza na wananchi katika ziara ya mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi aliyoifanya katika wilaya hiyo kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wanachama wa chama hicho kwenye mkutano wa hadhara.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa chama cha Mapinduzi ‘CCM’ wa kata ya Mikinguni wilaya ya Pangani wakiwa katika mkutano wa mwenyekiti wa chama hicho mko wa Tanga Rajab Abdulrahman uliofanyika January 23,2024,
Mradi wa maji ulioghalimu zaidi ya shilingi Milion 500 unaotekelezwa na mamalaka ya maji vijijini RUWASA wilaya ya Pangani ambao ulitembelewa na kukaguliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman hivi karibuni alipofanya ziara yake
Baadhi ya wanachama wapaya wa chama cha Mapinduzi waliohama kutoka vyama vya upinzani katika wilaya hiyo wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman akimkabidhi kadi ya CCM mmoja wa wanachama wapya waliohamia kutoka vyama vya upinzani.
Post A Comment: