Na Joel Maduka ; Geita

Kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa mhasibu wa kanda ya ziwa wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ,Upendo Furaha Peneza  na kurudi chama cha mapinduzi CCM , wanachama  481 wa vyama vya upinzani ambao walikuwa ni wafuasi wake wameamua kuungana naye pia na kujiunga na chama cha CCM.

Wanachama hao wamepokelewa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita , Barnabas  Mapande kwenye viwanja vya Kata ya Kasamwa ambapo ndipo ulipofanyika Mkutano wa kuwapokea.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CCM wilaya Barnabas Mapande amewataka wanachama hao kuwa na moyo wa uvumilivu na kuepukana na siasa za matusi ambazo zimekuwa aziwajengi watanzania.

“Ndugu zangu niwaambie ukweli kuwa Upendo Peneza anakuja na watu aliokuwa nao na mimi niwaambie ndugu zangu mchungaji mwema wa kondoo umfuata mchungaji wao sasa kwanini wengine wasimfuate Upendo Peneza”Barbabas Mapande Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita.

“Wale ndugu zetu wamekuwa na wasi wasi kuwa wataanikwa maovu yao nataka kuwaondoa shaka kuwa Peneza ajakulia kwenye familia ya matusi awezi kuwatukana wala kuwakashifu wao wawe na amani tu aliondoka amerudi Nyumbani sasa kwanini sisi tusimfanyie sherehe wao wawe wavumilivu tu Chama kipo kazini”Barnabas Mapande Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya geita

Naye Upendo Peneza ambaye alijiunga na CCM Tar 22 January 2024 ,amesema kuwa yeye hayupo tayari kushiriki siasa za kuwadanganya watu na kwamba amekuwa siku zote akisimamia ukweli na kuachana na uongo.

“Niliona kundi nililokuwepo siliwezi na sikuwa tayari kuwaragai watanzania na kuonekana natumika kwenye kundi ambalo linasiasa zisizo za ukweli mimi ni mwanachama wa ccm nimechagua kundi hili sababu limekuwa likisimamia ukweli na mimi nitasema ukweli siku zote wala sitakaa kimya kwa hofu ya  kumuogopa mtu yoyote”Upendo Peneza Mwanachama wa CCM.

“Ninajua wengi watasema maneno mengi mimi kuhamia ccm nataka niwaambie mimi sikuongwa na mtu kuingia CCM ukweli wa dhati mimi ndio niliwatafuta viongozi wa Chama cha Mapinduzi na kuwaomba wanikaribishe CCM sasa mtu umeomba kweli utakuwa tena umeongwa tuachaneni na maneno ya uragai ambayo yanasemwa”Upendo Peneza Mwanachama wa CCM.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Chacha Wambura ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuwa tayari katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kukichagua chama cha mapinduzi CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji.


Share To:

Post A Comment: