Zaidi ya wadau 2000 wa maendeleo kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wanatarajia kukutana mkoani Mwanza kwa ajili ya kongamano la siku mmoja kuzungumzia mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mratibu wa kongamano hilo linaloitwa Mafiga ya Rais Samia, Alloyce Nyanda, amesema litafanyika Mkutano Machi 30, mwaka huu ukumbi wa Kwa Tunza.
Amesema lengo kuu ni kuzungumzia miaka mitatu ya Rais Samia kwa kutoa tathmini iliyo huru kwa kuhusisha makundi huru katika jamii Kanda ya Ziwa.
Post A Comment: