Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa anaewakilisha kundi la vijana kutoka Viti vitatu Tanzania Bara Bi, Lulu Mwacha (MNEC) ametoa pikipiki Saba zenye thamani ya Shilingi milioni 21 kwa viongozi wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa wilaya saba za Mkoa wa Arusha lengo likiwa kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi kwa kuwafikia zaidi wanachama na wananchi hususani kundi la vijana na makundi mbalimbali katika maeneo wanayoyasimamia.

Akitoa Pikipiki hizo amewataka viongozi hao kwenda kuchapa kazi na kwenda kuyasemea yale yote mema yanayofanya na Chama cha Mapinduzi na kuendeleza gurudumu la kuchapa kazi kwa ufanisi kwa wanachama wote wa chama na wananchi wa eneo husika.

"Ni wajibu wangu kuwasaidia vijana wote waliopo ndani ya chama cha Mapinduzi na wale ambao sio wanachama

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM  Mkoa wa Arusha Thomas Loy Sabaya amempongeza MNEC Bi Lulu kwa kuwa mfano kwa kutoa usafiri ili kuwapunguzia usafiri viongozi hao ili waweze kushuka chini katika ngazi za matawi na mashina kwenda kusikiliza kero za vijana na kuwaeleza yale yote yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Haasan.

"Viongozi hawa wa vijana wakishuka kule chini na kwenda kuyaeleza yale yote mema yaliyofanya na serikali yetu sambamba na fedha zote za mirdi zilizoletwa katika maeneo yao na hakika watakwenda kutupa kura za kutosha na tutashinda kwa kishindo kikubwa ambacho hakijawaki kutokea " Aliongezea Sabaya

Hata hivyo Bi Lulu amesisitiza kuwa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu wa 2025 pikipiki hizo zitakwenda kutumike kama nyenzo ya kurahisisha ushindi wa chama katika vijiji, vitongoji na mitaa yote ndani ya Mkoa wa Arusha.





















Share To:

Post A Comment: