Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Patience Ntwina (kushoto) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi Mtendaji wa MISA TAN Bi. Elizabeth Riziki baada ya kutia saini mkataba wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.
Mwenyekiti wa bodi na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Amina Talib Ali akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa MISA TAN Bi. Elizabeth Riziki (kushoto) baada ya kutia saini mkataba wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.
****
Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wamesaini mkataba wa miaka mitatu (2024- 2027) wa ushirikiano makubaliano ya kufanya kazi kwenye maeneo mbalimbali ya haki za binadamu na hasa haki za waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla.
Hafla ya utiaji saini Mkataba huo imefanyika leo jijini Dodoma
na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa bodi na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Amina Talib Ali, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Mohamed Khamis Hamad, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Patience Ntwina, Makamishina, wakurugenzi wa tume na kwa Upande wa MISA TAN, Makamu Mwenyekiti wa MISA TAN Bw. James Marenga na Mkurugenzi Mtendaji wa MISA TAN bi. Elizabeth Riziki.
Post A Comment: