Na Ashrack Miraji Same
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafii amesema amefurahishwa na kitendo cha Joseph Mushi kuamua kumuunga mkono Rais wa Tanzania kwa kujenga zahahati Kibosho itakayokuwa msaada kwa wananchi hao.
Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi Wakati akikata utepe kuzindua rasmi Zahanati mpya ya Matela iliyojengwa na mdau wa maendeleo, Joseph Mushi katika kijiji Cha Singa wilayani Moshi mkoani kilimanjaro.
"Niseme familia ya Matela imekuwa ni familia ya mfano wa kuigwa katika Taifa letu,Mambo haya yanafanywa na watu wachache sana ,hili jambo walilofanya kwa kukamilisha zahanati Kwa ajili ya Wananchi wa kijiji hiki na vijiji jirani itakuwa ni historia kubwa na haitoweza kufutika.Wananchi wataendelea kunufaika na huduma hii ya matibabu katika zahanati hii," amesema
Boisafi amesema ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameweka bayana mambo yatakayofanyika kwa miaka mitano kutoka 2020 -2025 ikiwa ni pamoja na utoaji huduma ya Afya kwa jamii jambo ambalo limekuwa likipewa kipaumbele kwa nchi nzima na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Samia Suluhu Hassan.
Amesema jambo alilolifanya mdau huyo wa maendeleo ni la kuigwa ambalo linaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Tanzania ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na familia hiyo katika masuala huku akitoa wito kwa wananchi wa Kibosho waliopo maeneo mbalimbali waakumbuke kuijenga kibosho.
Akizungumza kwa niaba ya familia, Msemaji wa familia,Ibrahim Mushi amempongeza na kumshukuru kijana wao kwa kutimiza ahadi yake kwa kushirikiana na serikali ya CCM kwa kujenga zahanati hiyo itakayowanufaisha wananchi wa kibosho.
"Niseme tu hii zahanati siyo ya familia ya Matela hii zahanati ni wananchi wote ambao wanaishi maeneo haya na maeneo jirani bila ya kubagua jinsia ya mtu au Dini na kabila hii zahanat hipo Kwa ajili ya Wananchi wote lengo letu ni kumuunga mkono Mhe Rais wa Jamuhur ya muungano wa Tanzania Mama yetu kipenz Dkt Samia Suluhu Hassan Amesema Mr Ibrahim Mushi msemaji wa familia
Post A Comment: