Na Joel Maduka ,Kahama Shinyanga
Wanawake Halamashauri ya Msalala Wilayani Kahama wametakiwa kuwa wabunifu na kujenga tabia ya kukimbilia fursa mbalimbali zinapojitokeza ambazo zitawasaidia kujinyanyua kiuchumi na kuepukana na tabia ya kuendelea kuwa wategemezi kwa wanaume.
Wito huo umetolewa na mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi wakati akizungumza kwenye tamasha la Mwanamke Mwekezaji ambalo limefanyika kwenye Kijiji cha Kakola Kata ya Bulyanhulu.
Mbunge Iddi amesema ni vyema kwa wakina mama wakatumia fursa zilizopo kwenye Halmashauri ya Msalala kwaajili ya kuinuka kiuchumi kwani tayari miradi mbalimbali imeendelea kuwekezwa na kwamba wao kama wanawake kupitia vikundi vyao wanaweza kunufaika na miradi hiyo mikubwa ya kimakakati ikiwemo ya ujenzi wa Barabara pamoja na fedha za CSR ambazo zimekuwa zikitangaziwa tenda.
“Tulikuwa ziara Mkoani Mara tumeona mradi mkubwa wa mboga mboga na matunda tayari tumeongea na mgodi kuomba kupitia fedha za CSR tunakuwa na mashamba ambayo watapaitia vikundi ambavyo vitalima mbogamboga na matunda na kusambaza kwenye mgodi wetu wa Bulyanhulu pamoja na kwa makampuni yaliyomo ndani ya mgodi najua ukijiunga na kuanzisha vikundi mtakuwa wanufaika wakubwa wa mradi huu”Iddi Kassim Iddi Mbunge Jimbo la Msalala.
“Kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa Barabara ya Kilomita 73 niwaombe wakina mama msibaki nyuma kuchukua tenda kwani ni mradi ambao utadumu kwa miaka miwili nitashangaa kuona wanawake wengine wanatoka maeneo tofauti na wanapatiwa tenda nyie nawaomba muwe mstari wa mbele kuomba tenda nia yangu nataka kuwaona wanawake wa msalala mnanyanyka kichumi”Iddi Kassim Iddi Mbunge jimbo la Msalala.
Aidha kwa upande Mwingine Mbunge Iddi amewaunga wanawake hao kiasi cha Sh,Milioni moja ambacho kitasaidia kutunisha mfuko wa kikundi huku akiwahahidi kufadhili tamasha hilo kwa mwezi wa nane liweze kuwakutanisha wanawake wengi zaidi ambao watapatiwa elimu namna bora ya matumizi ya fedha na utunzaji wa fedha na mbinu za kuanzisha vikundi.
“Nataka kuona baada ya kuwa mmefundishwa na wawezeshaji ambao mmewataka wakina Nanauka nataka kuona yale ambayo mmeyazungumza mnayafanyia utekelezaji hili tunapokutana tusiwe watu wa kupiga porojo na kuachana na hapa nimetajiwa vikundi vinne najua kuna tatizo la ajira sasa kupitia kikundi cha Women Talk Group tunaomba wakinamama watano ambao wanauwitaji tutawaomba wapatiwa ajira na kampuni ya KASIPILIAN”Iddi Kassim Iddi Mbunge jimbo la Msalala.
Naye Mdau wa maendelo wa kata ya Bulyanhulu Mapungo Paschal Mapungo amesema chanzo kikubwa cha kuwawezesha wanawake ni kutokana na jitihada zao ambazo wamekuwa wakizifanya katika kujitafutia kipato cha kila siku ambacho nia yao ni kuinua maisha yao
Post A Comment: