MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amefanya kikao na wafanyabiashara wa mji wa Ikungi lengo likiwa ni kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi kupitia mamlaka ya Serikali.

Kero hizo ni pamoja na kuhusiana na

mazingira ya biashara baada ya stendi kuhamishiwa Kijiji cha Muungano ikiwa miundombinu bado haijakamilika, muda wa kufunga biashara kwa biashara za vinywaji na changamoto ya uongozi wao wa wafanyabiashara kutotimiza wajibu wao.

Akizungumza katika kikao hicho Mtaturu amewaomba wafanyabiashara kuendelea kushirikiana na vyombo vya usalama katika kulinda amani ili kuvutia wateja kuja kwenye mji wa Ikungi na hivyo kuwaongezea biashara na kukuza uchumi wa wananchi.

” Ndugu zangu niwashauri kuimarishe uongozi wenu ili iwe rahisi kuwasilisha changamoto zenu kwa pamoja kwenye mamlaka zinazosimamia biashara,”.amesema.

Amewahakikishia kuwa changamoto zao ikiwemo ya kurekebisha sehemu ya kuegeshea magari makubwa pembeni mwa barabara,kuweka vivuko sehemu palipojengwa Barabara za lami kwenye mitaa,kuweka milango kwenye vyoo vya stendi mpya na kuruhusu malori kupaki maeneo yaliyokuwa stendi ya zamani zitatatuliwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri afisa mazingira Richard Rwehumbiza amemshukuru mbunge kwa kuitisha kikao ambacho kinawakutanisha na wafanyabiashara wa mji wa Ikungi na kusema changamoto zilizoainishwa na wafanyabiashara watazifanyia kazi ikiwemo kuweka milango kwenye vyoo vya stendi mpya kwa kuwa fedha zipo.

“Kuhusu stendi ya zamani kurekebishwa kwa kuwekwa kifusi ili malori yaweze kuegeshwa nalo lipo kwenye mpango wa halmashauri,tunakuomba mbunge wetu utupe ushirikiano,”amesema.

Amewaonya wafanyabiashara kuendelea kuzingatia masharti ya leseni zao na kushirikiana kuweka mji safi kwani upo mpango wa kununua trekta na tela kupitia fedha za CSR kutoka kampuni ya Shanta Gold ili kusaidia ubebaji wa taka ngumu.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ikungi Suzana Kidiku amewaomba ushirikiano wananchi kuimarisha amani na usalama ili waweze kufanya biashara zao vizuri.

“Ndugu zangu niwaombe msiwalinde wahalifu ili Jeshi la Polisi liweze kutimiza majukumu yake,shirikianeni nalo kwenye

ulinzi shirikishi ambao ni mradi mmojawapo wa Jeshi la Polisi,”amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Wafanyabiashara Mwajuma Sambe amemshukuru mbunge kwa kuwasikiliza kero zao na kuaahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuweka mazingira mazuri ya kufanyia biashara na kukuza uchumi wa Ikungi.

#IkungiYenyeUchimiBoraInawezekana

Share To:

Post A Comment: