HALMASHAURI ya Bumbuli mkoani Tanga inatarajia kuokoa zaidi ya Sh.milioni 30 kwa mwaka kutokana na kuachana na matumizi ya mfumo wa karatasi kwenye vikao na kuhamia kwenye matumizi ya vishkwambi .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Baraka Zikatimu mara baada ya kugawa Vishkwambi kwa madiwani na menejimenti ya watumishi wa halmashauri hiyo.
“Kila mwaka tuna vikao vinne tulikuwa tunatumia zaidi ya Sh. million 40 kwa kutumika shajala (Stationary) lakini sasa kwa kununua hivi vishkwambi hivyo itatusaidia kuokoa fedha hizo ambazo tutapeleka kwenye shughuli nyingine za maendeleo, ” amesema Zikatimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Amir Shehiza amesema kuwa vishkwambi hivyo vitakwenda kuondoka changamoto ya ucheleweshwaji wa makablasha wakati wa vikao mbalimbali vya madiwani.
Wakati huo huo madiwani wa halmashauri hiyo wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa kuona umuhimu wa kuwanunulia vishkwambi hivo.
“Vishkwambi hivi vitaondoa changamoto tuliyokuwa tunakumbana nayo ya kucheleweshewa makablasha wakati Wa vikao vyetu, ” wamesema.
Post A Comment: