Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mariam Mwinyi amekutana na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Wake wa Marais wa Afrika (Organization of African First Ladies for Development (OAFLAD) , Dkt. Nardos Berhanu Ofisini kwake Ikulu Migombani tarehe: 12 Machi 2024.
Mama Mariam Mwinyi ni Mwanachama wa Taasisi hiyo yenye lengo la kujadili fursa na shughuli mbalimbali zinazoratibiwa kuwawezesha wake wa Marais kuwa viongozi bora na kusaidia kupata maendeleo katika nchi zao.
Post A Comment: