Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amezidi kuyafikia makundi mbalimbali kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi.
Miongoni mwa kikundi kilichofikiwa na mkono wa kheri ni kikundi cha Mwanamke Shujaa cha Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambacho kimechangiwa shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya kufugia mifugo mbalimbali yeye akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Kiwilaya Tukuyu mjini lengo ni kupata 20m kufanikisha malengo.
Mahundi amechangia shilingi milioni tatu,milioni mbili akiwa ameungwa mkono na rafiki zake.
Lengo la Mahundi ni kuhakikisha wanawake wanamiliki uchumi wao akitekeleza kauli mbiu yake ya “Twende Tukue Pamoja”.
Post A Comment: