
Mhe. Mchengerwa amekabidhi fedha hizo (09 Januari, 2024) kwa Waziri Jenista katika Ofisi yake ndogo Jijini Dar es salaam, ambapo amepokea fedha hizo kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mchengerwa amesema fedha hizo zilitolewa kwenye Mkutano wa Maafisa Elimu hao mwishoni uliofanyika Manispaa ya Morogoro ambapo Maafisa hao wametoa mchango wao kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwahudumia wananchi wa Hanang waliopatwa na maafa ya maporomoko ya mawe na tope.
“Maafisa Elimu kwa ushirikiano wao waliona umuhimu wa kuchangishana na kusaidia waathirika wa maafa yaliyotokea Hanang na kunituma nikukabidhi wewe Mhe.Waziri mwenye dhamana,”amesema.
Naye, Waziri Mhagama amewashukuru kwa mchango huo na kuunga mkono serikali katika kuhudumia wananchi hao na kwamba fedha hizo zimewekwa kwenye Akaunti ya maalum ya maafa iliyoko Benki Kuu.
Post A Comment: