Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mnzava leo Machi 14, 2024, imetembelea miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufungua utalii wa Malikale kwenye magofu ya Kisiwa cha Kilwa Kisiwani ikiwa ni juhudi mpya za kuongeza zao jipya la utalii huo.


“Tunaposema tunapongeza juhudi za Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kwa vitendo kama hivi. Hapa katika miaka hii mitatu Serikali yake imetoa fedha kuendeleza utalii wa malikale ikiwemo boti mpya ya kisasa ambayo watalii wanaweza kuona ndani ya maji, gati la kushuka abiria, jengo jipya la kufikia abiria na miundombinu mingine ambayo imechagiza idadi ya watalii kuongezeka hapa kutoka wastani wa 2900 hivi hadi 6,400. Haya ndio mafanikio yenye maono,” alisema Mhe. Mnzava.

Ziara hiyo pia walikuwepo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, Naibu wake, Mhe. Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na watendaji waandamizi kutoka Idara za Wanyamapori, Malikale na Misitu.


Share To:

Post A Comment: