Na Albano Midelo,songea
Tume ya Ushindani ( FCC) Nyanda za Juu Kusini imekamata bidhaa bandia na kutoa elimu ya bidhaa bandia kwa wafanyabiashara wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Bidhaa bandia zilizokamatwa ni ,vifaa vya kieletroniki na vya viwandani ambavyo vimeondolewa kwenye maduka hayo.
Mkuu wa Kanda Ofisi ya Tume ya Ushindani Nyanda za Juu Kusini Dickson Mbanga ameongoza operesheni ya kuondoa bidhaa bandia na kutoa elimu kwenye zoezi la ukaguzi wa bidhaa bandia katika maduka yaliyopo soko kuu la Songea Mjini.
Amesema lengo ni kuwapa elimu wafanyabiashara ili waweze kuepukana na matendo ambayo yanakiuka sheria ya ushindani pamoja na alama za bidhaa bandia.
“Wananchi wa Manispaa ya Songea watupe ushirikiano wa kutosha ili tuweze kukagua bidhaa zao kuwasaidia kuepukana na uuzaji bidhaa bandia katika maduka yao”, amesema Mbanga.
Kwa upande wake Afisa Biashara Mkoa wa Ruvuma Martin Kabalo amewaomba wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma watoe ushirikiana kwa wakaguzi wa bidhaa bandia ili waweze kutambua bidhaa halisi na bandia hivyo kuepusha madhara kwa watumiaji.
Naye Mfanyabiashara wa Manispaa ya Songea Hussein Dalla ametoa ushauri kwa wafanyabiashara wenzake kuacha kuuza bidhaa bandia ambazo zinaweza zinaweza kuleta athari kwa watumiaji.
Amewashuru wataalam kutoka Tume ya ushindani kuwapa elimu ya kutambua bidhaa bandia elimu ambayo imekuwa inatolewa kila baada ya miezi mitatu.
Wataalam kutoka FCC wapo mkoani Ruvuma kwa siku tano kwa lengo la kukagua vifaa bandia vinavyouzwa na kutoa elimu kwa wafanyabiashar ili kuepuka bidhaa bandia
Post A Comment: