Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. Phillip Mpango akizungumza na wadau mbali mbali wa ajira wakati akifungua mkutano wa saba wa washirika wa Kijamii wa Afrika ( ASP). Mkutano huo uulioandaliwa na Chama cha waajiri Tanzania ( ATE) umeanza leo Februari 7,2024 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kumalizika kesho Februari 8,2024
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
MAKAMU wa Rais Dkt. Phillip Mpango amezitaka nchi za Afrika kuchukua hatua za kutumia maendeleo ya teknolojia ili kukabiliana na ukosefu wa ajira pamoja na ka kuchochea uzalishaji na ukuaji wa uchumi barani humo.
Dkt.Mpango ametoa wito huo leo, Frebuari 6, 2024, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 7 wa Washirika wa Kijamii wa Afrika, uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amewashauri wajumbe wa mkutano kuitazama teknolojia ya akili bandia (AI) kama fursa na kwamba wasihofie.
“Katika eneo la maendeleo ya teknolojia, kunadhaniwa kwamba nafasi za ajira zitaathiriwa na AI. Pamoja na kuwa na dhana hiyo lakini teknolojia hiyo itatengeneza ajira mpya hasa zile zinazohitaji ujuzi wa kiufundi,” amesema
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 50 barani Afrika DKt. Mpango amesema kuwa muhimu kuendeshwe mafunzo yatakayoendana na mabadiliko ya teknolojia na kubaini sekta zenye fursa nyingi za ajira.
“Sekta ambazo akili bandia zinaweza kuongeza ajira ni kilimo ambapo AI inaweza kukuza utafiti wa kilimo kwa kubaini aina ya mbegu bora itakayomudu mabadiliko ya hali ya hewa ” alisema.
Akizungumza nje Mkutano huo , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzan Ndomba amesema mkutano huo utajikita katika masuala ya uzalishaji wa ajira kwa mada tofauti na kuja na mapendekezo.
Kwa upande wake, Roberto Suarez Santos, Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Waajiri (IOE) ameema, mkutano huo unatoa fursa ya kuunda suluhisho na mbinu za pamoja za kutatua changamoto za ajira kwa vijana na kwa ukosefu wa utulivu wa kijamii.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Said Wamba, amesema wakiwa wadau shirika lao linatarajia kujadili namna ya kuendeleza mijadala na midahalo yenye nia ya kuboresha uhusiano kati ya chama na waajiri kwa sababu ajira inamnufaisha kila mtu akiwemo mustakabali wa sekta ya ajira.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha waajiri Tanzania ( ATE) Suzanne Ndomba akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa saba wa washirika wa Kijamii wa Afrika ( ASP). Mkutano huo uulioandaliwa na Chama cha waajiri Tanzania ( ATE) umeanza leo Februari 7,2024 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kumalizika kesho Februari 8,2024
Picha ya pamoja.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Saba wa ASP uliofanyika Katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Post A Comment: