Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), imejipanga kukamilisha usimikaji mfumo wa kielektroniki wa Uendeshaji mashauri ya migogoro ya Kikazi katika ofisi zote Tanzania bara ifikapo Juni 30 mwaka huu.


Mfumo huo unalenga kurahisisha huduma za usuluhishi wa migogoro ya kikazi yenye lengo la kukuza sekta ya uwekezaji nchini.


Akizungumza Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA, Mhe. Usekelege Mpulla leo Januari 18, 2024 katika kikao cha kamati cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2023 na maazimio ya Bunge ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na taasisi zake.


Aidha, Mpulla amesema mfumo huu utasaidia usajili wa migogoro kwa wale walio mbali na ofisi za Tume kwani utawawezesha kusajili migogoro kwa njia ya mtandao na kupatiwa huduma kwa njia ya mtandao.


Mpulla amesema tayari mfumo huo umeshakwisha kusimikwa katika mikoa minne ambayo ni Mbeya,Songwe,Singida na Geita na pia wanaendelea na usimikaji katika mikoa mingine ambayo ni Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa,Songwe,Singida,Kilimanjaro,Tanga Tabora, Pwani na Shinyanga.

Share To:

Post A Comment: