Na Denis CHambi,Tanga.

CHAMA cha Mapinduzi 'CCM' Mkoa wa Tanga kimewaomba wananchi wa kijiji cha Mkambani kata  Boma Jimbo la Mkinga kuendelea kuwa na imani na  kumchagua mgombea  wake Ibrahimu Mamboleo  anayewania Udiwani  kwa tiketi ya chama hicho ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.


Uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata ya Boma Jimbo la Mkinga mkoani Tanga unatarajiwa kufanyika March 20,2024  ambapo vyama viwili pekee ndivyo  vilivyoingia kwenye kinyang'anyiro vikiimamisha wagombea wake  ambavyo ni Chama Cha Mapinduzi 'CCM'  kipitia kwa Ibrahim Mamboleo na Chama Cha ACT wazalendo kipitia kwa mgombea wake   Mohammed Shega.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya  kujiuzulu kwa Ibrahim Mamboleo aliyekuwa diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya  Chama Cha Wananchi 'CUF' ambapo baadaye alijiuzulu  na kuhamia CCM ambacho kilimpilatia ridhaa ya kugombea tena  ili kurudi   kwenye nafasi hiyo kwa chama tawala.

Akizungumza kwenye Kijiji Cha Mkambani kata ya Bomba wilayni Mkinga  katika kampeni za kumnadi mgombea huyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Rajabu Abdulrahman amesema kuwa  chama hicho kimejidhatiti kuwaletea Wananchi maendeleo katika huduma  mbalimbali za kijamii kikitekeleza ilani yake kwa vitendo. 

Alisema suala la upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo ya maji Safi na salama bado ni ya kusua sua hivyo ni wakati sasa wa kwenda kuisimamia serikali kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa wananchi kwa asilimia 85 ifikapo mwaka 2025 hii ikiwa ni sambamba na utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

"Tanga Taifa letu lipate Uhuru na kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa , ni Chama tawala  Cha CCM pekee ndicho kimewaletea wananchi maendeleo, hakuna Chama kingine chochote kitakachokuja kumkomboa mwananchi hususani wa hali ya chini"

"Sasa hivi bado tupo ndani ya utekelezaji wa ilani ya chama chetu cha Mapinduzi tukiahidi huwa tunatekeleza kwa vitendo hatupo kwaajili ya kuwadanganya wananchi ili tutakapokuja kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 kwenye suala la huduma za jamii tuwe tumetekeleza kwa hatua kubwa"

Aidha kuelekea uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika mwaka huu  wa 2024  Mwenyekiti huyo aliwaomba wananchi kuwachagua wagombea  watakapitishwa na Chama hicho ambapo wameahidi kwenda kuunda serikali imara na kuwasimamia viongozi wake wa chini ili  kuhakikisha wanawajibika ipasavyo.

"Mtakapo tupa kura tutaunda serikali kuhakikisha upatikanaji wa maji maeneo ya vijijini mpaka itakapofika 2025 upatikanaji wake itakuwa no asimilia 85 hii maana yake ni kwamba tunaichukua ilani yetu tunaangalia Yale tuliyoahidi katika wilaya ya Mkinga na tunakwenda kuyatekeleza kwa vitendo kuayatoa maji katika chanzo Cha mto Zigi na kuja na kuja kwenye Jimbo la Mkinga na vijiji vyake vyote"  alisema Abdulrahman.

Share To:

ABDULLMAKAVELL

Post A Comment: